Gari la shule laua wanafunzi 8, Rais Samia atoa pole

Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Mtwara

RAIS Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na taarifa ja ajali iliyosababisha watu 10 kupoteza maisha baada ya gari la shule kutumbukia shimoni.

Ajali hiyo imetokea leo baada ya gari lenye namba za usajili T 207 CTS Mali ya shule ya Msingi King David kutumbukia shimoni huko Mtwara Mikindani.

Rais Samia ametoa pole kwa wafiwa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu hao.

Kamanda wa Polisi Mtwara Nicodemus Katembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.