Idara ya Hali ya Hewa nchini India imeonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na wimbi la pili la joto kali katika muda wa wiki tatu, ikiwemo maeneo ambayo mamilioni ya watu wanatazamiwa kupiga kura katika uchaguzi wa wiki sita.

Idara ya Hali ya Hewa nchini India imeonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na wimbi la pili la joto kalikatika muda wa wiki tatu, ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo mamilioni ya watu wanatazamiwa kupiga kura katika uchaguzi wa wiki sita.

Idara ya hali ya Hewa ya India imeelezea “wasiwasi wa kiafya wa wastani” kwa watoto wachanga, wazee na wale walio na magonjwa sugu, na kuwashauri wakaazi wa majimbo hayo kuepuka kukaa kwenye maeneo ya joto. Mji mkuu waNew Delhi unatarajiwa kuwa na viwango vya juu vya joto vya 45C mwishoni mwa juma, kulingana na utabiri.