Skip to main content

JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine
  • Home
  • Kitaifa
    • Biashara
    • Siasa
    • Uchumi
  • Kimataifa
  • Makala
    • Siasa
    • Uchumi
  • MCHANGANYIKO
  • Michezo
  • Burudani
  • Kazi/Ajira
  • Gazeti La Jamhuri
    • Sitanii
    • JAMHURI YA WAUNGWANA
    • Nyundo ya Wiki
June 8, 2018
Kitaifa

Jeshi la Zima Moto Yapewa Tuzo ya Heshima

Jamhuri Comments Off on Jeshi la Zima Moto Yapewa Tuzo ya Heshima

JESHI la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo.

 

Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es Salaam.

 

Akizungumza Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho alisema, anaishukuru taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.

 

Andengenye, amezitaka taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.

 

 

Ni vyema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundombinu hiyo, wakumbuke kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.

 

Tuna changamoto kubwa kwa upande wa visima hivyo, kwa hiyo kampeni yetu ya kufufua na kuongeza visima hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji kazi katika fani yetu. Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha miundombinu hiyo inarudi na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji inapo jengwa.

 

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania, Muhammad Shaban alisema wamechukua uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na kuona mchango mkubwa wa Jeshi hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema wataendelea kutoa ushirikiano na Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma. “Tupo tayari kushirikiana na Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo fire hydrant zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam.”

 

“Kampeni ya kufufua fire hydrant imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa jamii kwani zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata maji eneo la karibu majanga ya moto yanapotokea.”

Post Views: 404
JESHI LA ZIMA MOTO
Previous Post Makundi ya Timu 16 Ligi ya Timu za Vijana Zatajwa
Next Post Viatu havibani, havipwayi vinatosha Na Angalieni Mpendu “Kweli nimeomba nipumzike kwa sabab
Posted By

Jamhuri

  • Serikali juboresha maendeleo ya raslimali watu kazini
  • Waziri wa Ardhi awaasa wahitimu Arimo kujiepusha na matendo maovu
  • Serikali itahakikisha miradi yote ya umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima – Chongolo
  • Ujenzi wa jengo la kituo cha mafunzo ya kuongeza thamani madini ya vito waanza Arusha
  • Uzalishaji maji washuka kutoka lita milioni 270 hadi lita 50 kwa saa

Habari mpya

  • Serikali juboresha maendeleo ya raslimali watu kazini
  • Waziri wa Ardhi awaasa wahitimu Arimo kujiepusha na matendo maovu
  • Serikali itahakikisha miradi yote ya umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima – Chongolo
  • Ujenzi wa jengo la kituo cha mafunzo ya kuongeza thamani madini ya vito waanza Arusha
  • Uzalishaji maji washuka kutoka lita milioni 270 hadi lita 50 kwa saa
  • Polisi wahimiza wananchi kuepuka vitendo vinavyoashiria vurugu
  • Manispaa Kibaha yamkabidhi baiskeli maalum mwanafunzi mwenye ulemavu
  • Nchimbi: Taifa limepata pengo kuondokewa na Jenista Mhagama
  • Rais Samia amlilia Jenista Mhagama
  • Tanzania kunufaika na zaidi ya USD milioni 15 kutatua changamoto za mazingira
  • Samia aokoa maisha ya wana Bukombe
  • Rais Samia amteua Mkurugenzi Mkuu PSSSF
  • RC Kunenge akemea ukiritimba unaokwamisha uwekezaji na huduma kwa wananchi
  • Chobo ataka ushirikiano wa kuchochea maendeleo
  • Mbunge wa Peramiho Jenista Mhagama afariki

Copyright 2024

Designed by JamhuriMedia