Na Jovina Massano
TANZANIA na Norway yabainisha mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na namna bora ya uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kukabiliana na janga la taka za plastiki.
Mikakati hiyo imejadiliwa jijini Oslo
na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mhe. Mhandisi Hamad Masauni pamoja na Bw. Andreas Bjelland Eriksen ambae ni waziri wa Hali ya hewa na mazingira nchini Norway yenye kuonyesha ushiriki wa Tanzania katika COP30.

Katika mazungumzo hayo Mhandisi Masauni amemweleza jitihada za Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi, alimweleza Bw. Eriksen kuwa Tanzania imejipanga kuhifadhi Mazingira kwa kuja na mipango na makatazo mbalimbali ikiwepo agenda ya Nishati Safi ya kupikia na kuhifadhi mazingira kwa kuja na mpango na makatazo mbalimbali ya matumizi ya nishati ya kuni na mkaa sambamba na vibebeo vya plastiki.
Ameendelea kueleza kuwa hivi sasa Tanzania imejipanga kupunguza matumizi ya Nishati isiyo salama ya kupikia kwa kuweka programu za mpito kwa kutoa makatazo ya matumizi ya kuni na mkaa katika taasisi zimaazozalisha watu zaidi ya 100 kuanzia 2024.
Tanzania imeazimia kuhakikisha Ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wameshaacha matumizi ya Nishati isiyo salama ya kupikia na kutumia nishati Safi ya Kupikia.
Aidha Waziri Masauji, alimweleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika na Duniani kote.
Ameongeza kuwa Tanzania imetoa katazo la matumizi ya plastiki (Vibebeo) na kuainisha tofauti ya vibebeo na vifungashio.
Kwa upande wake Waziri Eriksen amesema kuwa COP30 ni fursa adhimu kwani kila nchi duniani itapata fursa ya kuwasilisha taarifa yake ya tatu ya mchango maalum wa Taifa(Nationa Determined Contribution’-NDC.)
“Nina imani kuwa pamoja na taarifa hizo kuna baadhi ya nchi zitakuwa zimetimiza adhma zao na baadhi kutotimiza hivyo COP30 itatoa fursa ya kuona nini kifanyike ili kuziba mapengo hayo”, amesema Bw. Eriksen.
Aidha ameleza kuwa kwa kufanya kazi kwa mashirikiano baina ya mataifa mbalimbali ni matarajio yake kuwa ahadi ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi-Fedha za Marekebisho ‘(Adaptation Finance’) itaongezeka mara tatu katika mfuko wa Ubadilishaji. ‘(Triplering Adaptation fund’).

Hivi sasa Serikali ya Norway inafanyia kazi upatikanaji wa fedha kwa ajili ya masuala ya Mazingira na tayari wana Mfumo wa utekelezaji wa Artice 6 ambao unawasaidia katika utekelezaji wa miradi jumuishi, ili kuwa na lengo la pamoja na hivyo kuibua fursa mpya.
Article hiyo inalenga kuibua fursa mpya hivyo Tanzania ikiwa mwenyekiti wa kikundi cha wafanyabiashara wa Afrika(‘ African Group of Negotiators’- AGN) inaweza tumia fursa hiyo kuzishawishi nchi hizo kutambua fursa zilizopo na kuzitumia kwa mapana zaidi.
Kwa taka za plastic Waziri Eriksen ameeleza kuwa kuna umuhimu wa majadiliano ya kina kuhusu taka hizo kwani zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku ni muhimu mataifa yakashirikiana kukabiliana na janga hili.