Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema Kupitia ( Public -Private Partnership ) PPP, Serikali inapunguza mzigo wa kifedha na kiutendaji huku ikihakikisha Miradi ya Maendeleo inakamilika kwa wakati.
Kafulila ameyabainisha hayo Jijini Dar es Salaam mapema leo Mei 27, 2025
wakati akiwasilisha mada katika Kongamano la kitaifa kuhusu ushirikiano Kati ya sekta ya umma na Binafsi lenye mada kuu dola,masoko na uhamasishaji mitaji, nafasi ya Ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kufikia malengo ya dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.

Kafulila aliwasilisha mada inayosema nafasi ya PPP katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Amesema ni muhimu kuwa na PPP hasa katika ulimwengu wa sasa kwani kupitia PPP Miradi ya Maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
“Dhana ya PPP imelenga kuisaidia Serikali kukuza uchumi na kutoa huduma bora kwa wananchi”amesema Kafulila.
Ameongeza kuwa PPP ni muhimu kwa ustawi wa Taifa si tu kusaidia kuvuta teknolojia mpya, bali pia kuleta ufanisi wa kiutendaji .
Kwa upande wake mwanasiasa mkongwe nchini, Profesa Anna Tibaijuka akichagia mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PPPDavid Kafulila amesema pesa hazitokani na Serikali, bali hutoka kwa wananchi ambao ndio chanzo kikuu cha rasilimali.

Amesema kuwa mfumo wa PPP ni nguzo muhimu kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuwa unaleta uwazi na kuwahusisha wananchi moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“PPP siyo tu njia ya kuimarisha uchumi, bali ni utamaduni wa kushirikiana kwa uwazi, jambo linalowezesha miradi mikubwa kujadiliwa bungeni na kupewa kipaumbele”amesema
Naye Dkt Milanzi Mursali kutoka Tume ya mipango amesema kisheria ndio inajukumu la kuandaa dira na kwa Sasa wapo katika hatua za mwisho wa maaamuzi.
Aidha amesema Kupitia dira ya 2050 inapenda kuona Serikali za mtaa zinafanya maamuzi pasipo kutegemea Serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Naye Mhadhiri Mwandamizi kutoka Taasisi ya Uhasibu Arusha, Dkt. Kafigi Jeje ametoa wito kwa watendaji wa halmashauri zote nchini kuchukua hatua thabiti katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi.


