Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe ameeleza kuwa taarifa za kanisa hilo kukwepa kodi zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hazina ukweli na kuwataka waumini wake kutokubaliana nazo.

Askofu kakobe ailyaeleza hayo jana Jumapili, Februari 25, alipokuwa akiwahubiria waumini wake katika ibada iliyofanyika kanisani hapo Mwenge, jijini Dar es Salaam na kuwataka waumini hao kuzikataa taarifa hizo kwani zimejaa siasa ndani yake.

Taarifa hiyo ya Kakobe imekuja ikiwa ni siku nne tu zimepita tangu TRA kutoa ripoti ya uchunguzi waliyoifanya kuhusu mali zinazomilikiwa na kanisa hilo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Taasisi za Benki nchini, Chars Kimei aliionya Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusiana na kuweka hadharani taarifa za kifedha za wateja na kueleza jambo hilo linatishia usalama pamoja na uaminifu katika taasisi hizo.

Please follow and like us:
Pin Share