Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar

Kuelekea mchezo wa Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba Jumamosi hii, Afisa habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe ametangaza mchezo huo kuwa ni maalum kwa Wazee wote wa Yanga.

Akizungumza na wanahabari leo, Kamwe amesema kwa kutambua ukubwa, umuhimu na upekee wa mchezo huo wa Jumamosi, wao kama Yanga wameamua mchezo uwe maalum kwa ajili ya wazee wao.

“Tungeweza kumpa mchezaji au kiongozi hii mechi, lakini tumeileta kwa wazee, tunawaomba waje kwa wingi, lakini tunaamini dua zao zitakuwa silaha na kinga kwa wachezaji wetu” amesema Kamwe.

Aidha Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani siku hiyo ili kuwapa nguvu wachezaji wao, huku akiwasihi kuacha tabia ya kuwafuata wachezaji mitandaoni kuwapa presha ya mchezo huo.

By Jamhuri