Klabu ya Machester United iko mbioni kupigwa mnada na kuwa chini ya mmiliki mpya mara baada ya wamiliki wa klabu hiyo ambao ni familia ya Glazers kukubali kuiuza.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Novemba 23, 2022 kwenye tovuti rasmi ya Manchester United imeelezwa kuwa klabu hiyo itauzwa na itajikita zaidi katika uwekezaji na kuboresha baadhi maeneo kuanzia miundombinu, uwanja pamoja na kupanua kukuza na kuiamarisha mapato yake.

"Kama sehemu ya mchakato huu, Bodi itazingatia njia mbadala zote za kimkakati, ikijumuisha uwekezaji mpya katika klabu, mauzo, au mambo mengine yanayohusisha Kampuni."

 "Hii itajumuisha tathmini ya mipango kadhaa ya kuimarisha klabu, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa viwanja na miundombinu, na upanuzi wa shughuli za kibiashara za klabu katika kiwango cha kimataifa, kila moja katika muktadha wa kuongeza mafanikio ya muda mrefu ya klabu ya wanaume, wanawake na akademi." Imesema Klabu hiyo

Zinazohusiana
       -Ronaldo afungasha vilago Manchester United

Uamzi huo unafuata mara baada ya klabu hiyo kutangaza kuchana na nyota wake Cristiano Ronaldo ikiwa ni kutokana na maneno aliyoyasema Ronaldo kuonekana kuwa ya kichochezi.

Ikiwa ni Siku chache zimepita tangu Cristiano Ronaldo afanye mahojiano na Pers Morgan ,Talk Tv na kudai kusalitiwa na klabu lakini pia alisema wamiliki wa kalbu hiyo familia ya Glazers wanajali pesa zaidi kuliko timu.

Klabu ya Manchester United inawafuasi wengi duniani na imekuwa chini ya umiliki wa familia ya Glazier kutoka Marekani kwa takribani miongo miwili.

By Jamhuri