Mbunge wa Kwimba, Shanif Hirani Mansoor (CCM), amesema ameshaanza kushughulikia ujenzi wa mabwawa ya maji katika kata kadhaa jimboni humo.

Wakazi wa Kwimba wanachangia maji na mifugo kwenye mito na madimbwi. Kata za Mwakilyambiti, Ngudu, Kikubiji na Bupamwa zitanufaika.


Diwani wa Kata ya Mwakilyambiti, Sylvester Budila (CCM), ameiambia JAMHURI kwamba wakazi wa jimbo hilo wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji kwa zaidi ya miaka 50 sasa.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Seleman Mzee, amesema pamoja na uchimbaji wa mabwawa hayo, Serikali nayo inaendelea kujizatiti kuhakikisha kero ya maji inabaki historia wilayani humo.


Kwa upande wake, mkazi wa mji wa Ngudu, Bahati Maduhu, ametilia shaka jitihada hizo zinazofanywa na mbunge pamoja na Serikali, akisema zinaweza kuwa zimamoto au mbio za sakafuni.


Please follow and like us:
Pin Share