Rais John Pombe Magufuli alipokutana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa Ikulu.

 

WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema), Edward Lowassa amekutana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho wa alichozungumza na Rais Dkt. John Magufuli juzi Januari 9, alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Kwa mujibu nwa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa na taarifa nyingi za kuupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake.

Please follow and like us:
Pin Share