Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utiaji saini mikataba 20 ya ukarabati na ujenzi wa miradi ya umwagiliaji baina ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji chini ya Wizara ya Kilimo na Wakandarasi jijini Dodoma hapo kesho.

Mikataba hiyo ni ya ujenzi na ukarabati wa Skimu 14 pamoja na miradi sita (6) ya usanifu wa kina na upembuzi yakinifu ili kampuni zilizoshinda zabuni ziweze kuanza zoezi la utekelezaji wa miradi hiyo kupitia mikataba husika.

Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na skimu ya Itping iliyopo wilaya ya Njombe mkoani Njombe, Skimu ya Mahiga iliyopo wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Skimu ya Msange iliyopo Wilaya ya Singida mkoani Singida, Skimu za Ndungu na Kihurio zilizopo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, ujenzi wa Bwawa na Skimu ya Luiche katika Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.

Kwa upande wa usanifu wa kina na upembuzi yakinifu katika Bwawa la Kalupale lililoko wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, upembuzi yakinifu katika Skimu ya Ifakara – Idete iliyopo Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, eneo lingine ni Pamoja na Skimu ya Butonga – Nyamazuka, Igaka – Bundala na Isole Mkoani Mwanza.

Please follow and like us:
Pin Share