Na Kulwa Karedia,JamhuriMedia,Ruangwa

Waziri Mkuu Majaliwa Kasimu amesema changamoto nyingi zilizokuwepo ndani ya Wilaya Ruangwa zimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kupeleka fedha nyingi katika sekta mbalimbali.


Majaliwa ametoa kauli hiyo Septemba 24,2025 katika uwanja wa Maonyesho ya Madini wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Amesema kutokana na hali hiyo, wana Ruangwa wamemhakikishia kumpatia kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.


“Wananchi wanayo kila sababu kupiga kura zote kwako, waubunge na madiwani wa chama chetu kwa sababu umefanya kazi kubwa mno ndani ya Wilaya yetu ambayo ilikuwa na changamoto nyingi, sasa mambo yamekwenda vizuri karibu kila sekta,”amesema.


Anasema wilaya hiyo ilianza mwaka 1995, ilikuwa na upungufu mkubwa, lakini kazi
Imefanyika ambapo Rais alipeleka karibu sh bilioni 26.


“Changamoto nyingi zimepungua kwa kiasi kikubwa,shule za kutosha, mradi wa maji kutoka Nyangao kwenda mjini umekamilika.


Anasema kulikuwa na baadhi ya wakandarasi wanaojenga barabara wilayani humo walikuwa wanadai Sh bili 9 tayari wamelipwa fedha zao zote na kazi inaendelea.


Amesema serikali imetoa Sh bilioni 13 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nanganga ambayo ni muhimu kwa uchumi wa wilaya hiyo.


Amesema tayari Rais Samia ameridhia ujenzi wa tawi la Chuo kikuu cha Dar es Salaam wilayani humo kuhusu fidia ya wananchi waliokuwa wanadai, wamelipwa sh bilioni 2.


“Umetufanyia mambo makubwa kama haya, tunayo sababu kila sababu kukupigia kura za ndiyo, ndiyo maana nasema Ruangwa kwa maendeleo inawezekana.


“Wana Lindi tuna sababu za kuendelea kumchagua Samia, tujitokeze kupiga kura,”amesema.


Amesema Rais Sama ameanzisha ujenzi wa
bandari ya uvuvi ambayo itasaidia kuondoa changamoto kwa wavuvi.


Amesema ujenzi wa barabara ya Kibiti-Lindi ujenzi wake umeanza na unaendelea.
“Mheshimiwa Rais ulinituma nilikwenda Japan nikakutana na Waziri Mkuu tulikaa tukazungumza na kukubaliana fedha zinakuja kwenye miradi hii.


Amesema hali ya maendeleo katika mikoa ya Lindi na Mtwara ni inafanana, ndiyo maana Rais Samia ameamua kufungua fursa ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mtwara- Masasi hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma.


‘Umegundua ipo fursa nzuri umeamua kuanzisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mtwara- hadi Nyasa hii fursa kubwa mno kwa mikoa yote, kwa uchapakazi wako naamini mambo yote yatakamilika”amesema
Amesema hatua hiyo zinawapa kiburi wananchi wa Wilaya na mikoa hiyo kukupiga kura kwa wingi.


“Nimezungumza kila wilaya ya nchi hii nimepitia miradi yote, Rais ametekeleza, ipo iliyoanza na inayoendelea, nawahakikishia itakamilika,”amesema.


“Tumchague Samia ili aje akamilishe miradi yote hii, mambo makubwa yanakuja, tumchague ili akamilishe kazi hii kwa manufaa ya Taifa letu,”amesema.


Amesema mgombea ubunge wa Jimbo Hilo, Kaspari Limuya ndiye mbunge aje atafanya vizuri kama wananchi watampa uwezo wa kufanya kazi.


“Kila mmoja wetu piga kura za ndiyo kwa madiwani wa CCM ili aweze kufanya kazi za kuleta maendeleo,”amesema.