Mamia ya watu wanahofiwa kupotea baada ya boti iliyobeba wahamiaji kuzama pwani ya Libya.

Walinzi wa majini wa Libya wanasema kuwa watu mia tatu wameokolewa kutoka boti nyingine tatu zilizopata dhoruba.

Walioopona katika ajali hiyo ya majini wanasema kuwa walitumia masaa kadhaa ndani ya maji kabla ya kuokolewa.

Tukio hili ni la karibuni Zaidi kutokea tangu kuanza kwa mwaka mpya.

Zaidi ya wahamiaji sita waliuwa baada ya boti yao kuzama siku ya jumamosi, ikiwa ni ni tukio la mwanzo la vifo vya watu Mediterranean kwa mwaka 2018.

 

By Jamhuri