Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya wakiimba Wimbo wa Mshikamano (Solidarity Forever) kwenye Maadhimisho ya Siku wa Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.
Wafanyakazi kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi za umma na binafsi wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Maadhimisho ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambazo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.