Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Mawaziri Nane kujadili utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kilichofanyika katika kituo cha Mikutano cha Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Mabula Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ameongoza kikao cha Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta kujadili utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

Kikao hicho kilichofanyika Agosti 18, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kilihudhuriwa na Waziri wa Ulinzi Stergomena Tax, Waziri TAMISEMI Innocent Bashungwa, Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Khamis Hamza Chillo pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara za kisekta.

Katika kikao hicho Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ilipokea taarifa ya tathmnini ya kazi iliyofanyika katika mikoa 13 ya Tanzania Bara kutoka kwa timu ya wataalamu sambamba na kupokea mpango kazi wa utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri katika mikoa iliyosalia.

By Jamhuri