Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mbunge kutoka Embakasi Mashariki ya Kenya Paul Owino (Babu Owino) amewashauri Ngome ya Vijana chama cha ACT Wazalendo waikanushe kauli ya kuwa wao viongozi wa kesho bali waamini kuwa wao ni wa leo .

Ameyasema hayo leo Februari 29,2024 Jijini Dar es Salaa wakati akifungua uchaguzi viongozi ngome ya Vijana ambapo amebainisha kuwa vijana ndiyo wengi katika nchi yeyote hivyo lazima watoke wajipiganie .

Sambamba na hayo Babu Owino amewasisitiza vijana wote kuendelea kuwa waadilifu ili waweze kuaminika kushika nyadhifa za uongozi kwani hata marais walioongoza nchi za Afrika hadi kupata Uhuru walianza kama wao akitolea mfano Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Jomo Kenyata ,Kwame Nkuruma,Nelson Mandela .

“Siasa katika Bara la Afrika ni siasa safi inafaa kuleta watu pamoja kupunguza Ufisadi, umasikini, rushwa itakayotusaidia kijinasua katoka katika minyororo ya ukosefu wa ajira mimi nchini kwetu Kenya wapo asilimia 70 na walikuwa wakitumika katika kampeni huku wakiambiwa kuwa wao ni viongozi wa kesho hivyo tumeikataa hiyo kauli na sisi tumefungua macho kugundua kuwa tunanyang’a nywa sasa tunapambana kupata uongozi ili kutatue changamoto zinazoikabili nchi yetu” amesema Paul Owino.

Naye Mwenyekiti anayemaliza muda wake Ngome ya Vijana ACT Abduli Nondo ameshukuru kufanya kazi ya na vijana ambao wamekuwa wakijitolea kufanya kazi ya kujenga chama .

Awali Katibu wa ngome ya Vijana ACT Wazalendo Mwanaisha Mndeme amesema wajumbe waliohudhuria katika uchaguzi huo ni 122 kati ya 143 hivyo kwa idadi hiyo uchaguzi unakwenda kufanyika

Naye Adolf Shaibu Katibu Mkuu Chama cha ACT Wazalendo amemshukuru Paul Owino kuja kushirikiana nao katika shughuli hiyo ya uchaguzi Ngome ya Vijana ACT hivyo wanaamini kuwa nasaha hizo alizozitoa wanakwenda kuzifanyia kazi.