Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia amesema ana wasiwasi kwamba silaha zilizopelekwa nchini Somalia huenda zikaishia mikononi mwa magaidi. Haya yameripotiwa leo na shirika la habari la serikali ya Ethiopia siku moja baada ya meli ya kivita ya Misri kuwasilisha shehena kubwa ya silaha nchini Somalia.

Katika taarifa iliyotolewa jana jioni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilisema kuwa shehena ya msaada wa kijeshi ya Misri imewasili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, kusaidia na kuimarisha uwezo wa jeshi la Somalia.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa msaada huo unathibitisha jukumu kuu linaloendelezwa la Misri katika kusaidia juhudi za Somalia kuimarisha uwezo wa kitaifa unaohitajika kutimiza matarajio ya watu wake ya usalama, utulivu na maendeleo.

Uhusiano kati ya Misri na Somalia umeongezeka mwaka huu kutokana na hatua ya pamoja ya kutoiamini Ethiopia.

Mnamo mwezi Agosti, mataifa hayo mawili pia yalitia saini makubaliano ya pamoja ya usalama.

Please follow and like us:
Pin Share