Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mbeya
MAHAKAMA ya Wilaya Mbeya imemuhukumu Mfanyabiashara Benedicto Abel Matandiko wa Jijini la Mbeya adhabu ya kutofanya Kosa lolote la Jinai ndani ya miezi 6 baada ya Kutiwa hatiani kwa Makosa ya Kutokulipa Kodi Kinyume na Kifungu cha 83 cha Tax Administration Act, Kughushu kinyume na vifungu vya 333,335(1) (a) na 337 vya Kanuni ya Adhabu, Kuwasilisha nyaraka za Uongo kinyume na vifungu vya 342 na 337 vya Kanuni ya Adhabu na kosa la Kusababisha Hasara Mamlaka husika kinyume na Aya ya 10 Jedwali la 1 la Sheria ya Uhujumu Uchumi. Hukumu hii imetokana na Plea Bargaining Agreement ambayo imeingiwa kati ya DPP na Mshtakiwa.
Hukumu dhidi ya Mfanyabiashara Bw. Benedicto Abel Matandiko imesomwa September 16, 2025 kutokana na shauri la Uhujumu Uchumi Na. 12620/2025 lililokuwa katika Mahakama ya Wilaya Mbeya mbele ya Hakimu Mkazi Teddy Mlimba akishirikiana na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Sospeter Tyeah
Ilielezwa kuwa Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kughushi na kuwasilisha receipts za EFD zinazoonesha VAT ya Tshs. 6,279,864.39 akidai kwa Mbeya UWSA akionesha kuwa yeye amesajiliwa na TRA kama mlipa kodi kwa Njia VAT huku akijua kuwa siyo kweli kwani yeye Hana EFD Machine na wala Hajasajiliwa na TRA kuwa mlipa kodi kwa VAT.
Mbeya UWSA walimlipa Bw. Benedicto kiasi hiki cha Tshs. 6,279,864.39 wakijua yeye ni VAT registered na baada ya kulipwa hakuziwasilisha TRA na alizitumia kwa manufaa yake binafsi.
Mahakama imeamuru kurejesha kiasi chote cha Fedha Mbeya UWSA na kuamriwa atekeleze makubaliano yote yaliyomo kwenye Plea Bargaining Agreement.
