Katika sehemu ya kwanza ya makala hii, wiki iliyopita tulishuhudia eneo la Jeruzalem lilivyokuwa likikaliwa na Wafilisti na Wayahudi bila shida. Leo tunakuletea sehemu ya pili, inayoendeleza simulizi za chimbuko la mgogoro wa Waisrael na Wapalestina. Endelea…

Kwa mujibu wa masuala ya utamaduni – kulikuwa na kuhama kwa makabila mengi ya Waebrania kutoka Chaldea kwenda nchi ya  Kanaani- katika mwaka wa 1730 BC. Makabila ya Wahebrania hata hivyo, hayakujiimarisha katika nchi ya  Canaani,  na yalielekea Misri ambapo yaliishi chini ya utawala wa Pharaoh.

Zaidi ya hapo , kwa  mujibu wa masuala ya tamaduni za kale Wahebrania au Waisraeli waliondoka Misri – karne chache baadaye na kutapakaa katika Jangwa kwa miaka mingi. Katika  mwaka  wa  1200 BC , Waisraeli waliivamia nchi ya  Kanaani kutoka mashariki na kuivamia Jericho. Waliuharibu mji  na kuwafumusha wakazi wa eneo  lile.

Makabila ya Waisrael yalianza  kutapakaa katika nchi ya  Kanaani, mchakato ule ulikuwa wa taratibu na ulichukua kama karne mbili hivi. Waisrael hawakufanikiwa kuiteka nchi yote – kwa vile Wafilisti-( ambao ndiyo asili ya jina Palestina walidhibiti pwani ya Kusini na eneo la Kaskazini mwa Japho (Jaffa). Kwa upande mwingine, Wafoenisian walidhibiti eneo linalojulikana leo kama Galilaya Magharibi – hadi eneo la Kusini mwa Acco. Wafilisti walikuwa mara kwa mara katika vita na Waisrael- ambapo walipigana kwa zaidi ya miaka  200.

Kwa muda mrefu , baada ya uvamizi wa ardhi ya Kanaan, Waisrael  hawakudhibiti  himaya ya Kifalme wala serikali kuu. Waliishi kama makabila na walitawaliwa na majaji. Ilikuwa tu ni katika kipindi cha mwaka 1000 BC – ambapo Daudi alianzisha Himaya ya kwanza ya Wayahudi – Palestina.

 

Nini kilitokea kwa Wakanaan baada ya uvamizi wa Waisrael?

Baadhi ya maandiko katika Bibilia  yanadai kuwa Wakanaan waliteketezwa wote. Baadhi ya maandiko yanadai viinginevyo: Hivyo, Biblia inasema kwamba:

(Waamuzi 3:5 na 6) “Basi wana wa Israel wakaketi kati ya wa Kanaani hao Wahiti na hao Waamori na hao Waperizi na hao Wahivi na hao Wayebusi wakawaoa binti zao na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume na kuitumikia miungu yao.

Isisahaulike ya kuwa Biblia ni mchanganyiko wa historia, hekaya na mythology (dhahania) ya Wahebrania. Wanahistoria wa kisasa wanagoma kukubaliana na nadharia ya mauaji ya jumla ya Wakanaan au upandikizaji wa  kikatili  wa kundi la watu katika nafasi ya kundi  jingine. Inaonekana ya kwamba Waisraeli na Wakanaan, kwa kipindi fulani walichipua kwa pamoja na kuwa wamoja (kuishi sehemu moja).

 

Professor Adolphe Lods  anaeleza:

“Watu wa Israel katika himaya ya kifalme walikuwa ni mchanganyiko wa Wahebrania na Wakanaan, katika muktadha huu, chembe chembe za u- Kanaan zilikuwepo kwa kiwango kikubwa ….wakiwa wamestaarabika kwa kiwango kikubwa , Wakanaan.”

Ufalme wa Daudi ulidumu kwa chini ya miaka 80. Mnamo 922 BC baada ya kifo cha Solomon, uligawanyika katika ufalme wa Kaskazini  wa Israel na Ufalme wa Kusini  wa Yuda. Lakini  falme hizi mbili zilisambaratika moja baada ya nyingine. Ufalme wa Israel ulisambaratishwa na Wa-asyria mnamo 721 BC na watu wake Wakachukuliwa mateka tangu kipindi  kile Ufalme wa Israel ukafa.”

Kama ilivyokuwa kwa Ufalme wa Yuda iliteketezwa na Wababiloni mnamo 587 BC- na watu wake wakafanywa kuwa mateka. Hii iliwakilisha  mwisho wa Utawala wa Wayahudi – Palestina na hali hiyo ilielezwa katika  maneno yafuatayo; “Makabila 12 yaliondolewa na kwenda Caucasus, Armenia- na hasa Babylonia – na kupotea.

Hatimaye, mnamo 520 B.C Cyrus Mfalme wa Persia aliwaruhusu Wayahudi kurudi Palestina.  Si wote waliorudi, lakini wale waliorudi waliishi chini ya utawala wa Persian- na baadaye chini ya utawala wa Marcedonia na ule wa Rumi. Walipambana mara kwa mara dhidi ya watawala wao, lakini hawakutawala tena nchi.

Tangu wakati ule hadi karne ya 20, wakati u- zayoni ulikuwa na uwezo chini ya utawala wa Waingereza kupanga uhamaji  mkubwa wa Wayahudi (A massive Jewish -Migration) kuelekea Palestina – Wayahudi wachache waliikalia nchi.

 

>>ITAENDELEA.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa Anapatikana kwa:-

 (+255)784  142  137

(+255) 713 333141

Au  barua  pepe

[email protected]

[email protected]

By Jamhuri