150827102252-donald-trump-july-10-2015-super-169Mwaka huu taifa kubwa lenye ushawishi mkubwa katika ulimwengu wa leo, Marekani, watafanya uchaguzi wa Rais, kuchukua nafasi ya Rais Barrack Obama. 

Kule Marekani uchaguzi wao unafanyika mwezi Novemba, lakini madaraka wanakabidhiana tarehe 20 Januari ya mwaka unaofuata.

Wagombea kinyang’anyiro cha urais kule Marekani wanatoka vyama vile viwili; Chama cha Republican na chama cha Democratic. Wameshaanza kampeni za uchaguzi wao. Mpaka sasa mimi baada ya kufuatilia kwa karibu matamshi ya mgombea urais wa chama cha Repulican, nimekwazika kutoa maoni yangu. 

Huko nyuma, katika dunia yetu hii, kule Ulaya kuliwahi kutokea kiongozi anayefanana na huyu mgombea wa Republican. Mgombea huyu, Donald Trump, licha ya kuwa Gavana na Seneta wa Jiji la New York, ni jitu lenye ubabe, ana tabia za ubaguzi mkubwa wa rangi (racism) na ana chuki za udini.

Katika mikutano yake ya kampeni amewahi kutamka maneno ya kuchukiza. Amewahi kuwaita Waislamu kama wakuja wasio na haki ya kuishi nchini Marekani (unwelcomed immigrants in the USA). 

Wakati Papa Francis akizuru nchi jirani ya Mexico mwishoni mwa mwaka jana, Trump alisikika kutamka kuwa atakapojaaliwa kuwa Rais wa Marekani, atajenga ukuta katika mpaka kati ya nchi yake Marekani kutenganisha na Mexico ili kuzuia wahamiaji haramu kutoka Mexico wasimiminikie nchini Marekani. 

Kwa tamko lile, Papa alitoa angalizo kwa kusema, “wanadamu wanajenga madaraja ya kuwaunganisha na kamwe hawajengi kuta za kuwatenganisha” kuonesha hakubaliani na wazo lile la kujenga ukuta mpakani mwa Marekani na Mexico.

Mimi ninaingiwa na hofu kuwa Donald Trump akija kuwa Rais wa Marekani dunia itakuwa katika hali ya wasiwasi kweli. Ushirikiano na uhusiano wa kimataifa uliojengwa na Rais Obama utabomolewa. Hofu hii inanijia kutokana na matukio ya huko nyuma.

Historia inatuonesha kiongozi mmoja wa Ujerumani aliyekuwa na hulka kama hizi za Trump duniani palitokea Vita Kuu ya II mwaka 1939-1945.

Katika mikutano yake ya kampeni Trump, akipigwa maswali na waandishi, basi anajibu kwa namna ya kuwachanganya wasikilizaji na kutoa majibu tatanishi. Mathalani, wakati mwandishi Willi Rahn wa CBS News alipojaribu kutaka kujua huyu Trump yukoje alianza hivi, “Is Donald Trump confusing everyone on purpose?” Hajamwelewa bado na ndipo anachanganyikiwa na akasema “Donald Trump is trying to confuse us. Or maybe not; May be he’s  just perpetually confused himself”.

Kwa tafsiri yangu, mwandishi amejiuliza “Huyu mgombea ni mhadaaji au amechanganyikiwa au vipi?

Si huyo tu bali kuna mwandishi mwingine Ben Carson huyu alidhani wapo akina Trump wawili katika kugombea urais mwaka huu. Ndipo akamwelezea katika mkutano kwa maneno haya, “I believe there were two Donald Trumps- the insult-prone shown we’re all familiar with and a “cerebral” one we don’t”. Kwa tafsiri yangu ni hivi, wapo akina Donald Trump wawili – mmoja fedhuli tunayemfahamu na mwingine ni yule mwenye akili (cerebral) ambaye hatumjui.

Mgombea Donald Trump hapo hapo katika kikao alikubali kuwa inawezekana nyinyi mnaona akina Trump wawili lakini yeye ni huyo huyo Trump (soma hayo kutoka Guardian toleo No. 0462 la Jumapili, tarehe 3 Aprili, 2016 uk, 31) katika picha yake kwenye ABC News) amejigamba hivi “I don’t think here are two Donald Trumps. There is one Donald Trump”.

“It’s me, I am who I am”

Mgombea urais huyu namuona kuwa kiongozi asiyetabirika. Ana mawazo finyu na mwenye dharau kwa viongozi wa Afrika. Nimefikia kuandika haya baada ya kuona jinsi mgombea huyu Trump alivyowadhalilisha viongozi wetu wa nchi huru za Afrika kwa matamshi yake katika mkutano. 

Katika kujibu swali kutoka mwanahabari aliyetaka maoni ya mgombea huyu juu ya lile wazo la viongozi wa nchi huru za Afrika kutaka kujiondoa kutoka ICC (International Criminal Court) kule Hague, Uholanzi, Trump alitoa maoni yake namna hii nayanukuu hapa, “It is shameful for African leaders to seek exit from ICC. In my view, these leaders want to have all the freedom to oppress their poor people without anyone asking them a question”.

Hakukomea pale tu bali aliongeza kusema maneno mengine ya hovyo kuwakashifu viongozi wa nchi huru za Afrika kwa kutamka hivi namnukuu tena. “…. I think there is no shortcut to maturity and in my view Africa should be recolonized, because Africans are still under slavery. Look, at how those African leaders change constitutions in their countries so that they can be life presidents. They are all greedy and do not care about the common people….”( Future or Sunday News toleo No. 32227 la tarehe 27 Machi 2016 Uk. 7).

Baada ya kusoma maneno hayo nikajikuta nakwazika sana kutoa mtazamo wangu juu ya mgombea huyu anajifanya kuwaonea huruma wananchi katika Bara la Afrika ambavyo siyo kweli hata kidogo. Mzungu yoyote hawezi kumwonea huruma mtu mweusi isipokuwa tu pale bepari anapotaka kumnyonya huyo mtu mweusi.

Kwa tafsiri yangu isiyokuwa rasmi matamshi yale ya Trump yalimaanisha hivi. Kwanza alisema ni fedheha au ni aibu kwa viongozi wa Afrika kutaka kujiondoa kutoka ile Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa anavyofikiri yeye (Trump) eti viongozi hao wanataka kujitoa kwenye Mahakama ile ili wawe huru kuwakandamiza maskini wananchi wao pasipo kubughudhiwa na yeyote yule.

Halafu aliendelea kuropoka kuwa anavyojua yeye hakuna njia ya mkato katika kupevuka na kwa mtazamo wake, bara la Afrika angependa litawaliwe tena kikoloni. Anaona eti Waafrika wangali wanakandamizwa kitumwa tu. Viongozi wote wa nchi huru za Afrika ni walafi na wenye uroho wa madaraka. Akaelezea namna viongozi hawa wanavyobadilisha katiba katika nchi zao ilimradi waendelee kutawala maisha yao yote (yaani wawe marais wa maisha).

Mimi sikubaliani kabisa na matamshi hayo. Kadiri nikumbukavyo, nilipata kusikia tamko la urais wa maisha kutoka kwa rais mmoja tu humu Afrika. Huyu alikuwa ni Dr. Ngwazi Kamuzu Banda wa Malawi aliyediriki kujiita “life president” siku hizo. Hivyo siyo sahihi kuwajumlisha marais wote wa nchi huru za Afrika. Isitoshe kwa suala la kurekebisha katiba ili viongozi waendelee kutawala nchi kadhaa duniani wapo viongozi wanaotawala kwa ukiritimba namna ya huu unaoonekana hapa Afrika. Kwa nini hazungumzii utawala wa Cuba ambako tokea mapinduzi aliyomng’oa dikteta Batista mwaka 1959 mpaka leo 2016, miaka 57 ya tawala, ni ukoo wa Castro tu ndiyo unaotawala?

Si hivyo tu, wakati mzee Mugabe anagombea urais mara ya mwisho mwaka 2014, mwandishi mmoja wa BBC alimuuliza swali,“Vipi huwezi kupumzika na kumpisha mtu mwingine kutoka chama chako akagombea urais wa Zimbabwe?”

 

>>ITAENDELEA

1887 Total Views 2 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!