Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,
Dar es salaam
Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke kwa tiketi ya cha AAFP Yusufu Rai amewaomba Wananchi kumpa kura ifikapo Octoba 29,2025 kwa kishindo atakwenda kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa kero ya Wanafunzi kukaa chini Baadhi ya Shule ,kuongeza Majengo Kituo cha Afya Mtongani,Kujenga Miundombinu ya Maji Mvua ikinyesha yasikae muda mrefu.
Akizungumza na Wananchi wa Mtongani katika Kampeni zake Zilizofanyika Uwanja wa Mwembe Mkole Octoba 3,2025 Dar es salaam amesema NI wakati wao kufanya mabadiliko ili Mtongani ibadilike kwani ndiyo Kata yenye wakazi wengi Temeke lakini IPO nyuma kimaendeleo tangu Uhuru Hakuna Shule za Msingi bado wanafunzi wanakaa chini madawati ni machache Kituo cha kutolea huduma za Afya huduma ni hafifu ni masaa 12 tu Wataalamu wa Afya hakuna suala ambalo linasikitisha .

” Tumekuwa na wabunge walipita Temeke hawajawahi kuifikiria Mtongani wamekwenda kufanya Maendeleo kata wanazotokea Sisi wametusahau ukiangalia Sisi ndiyo wapiga kura tulio wengi sasa Mimi kijana wenu nimezaliwa hapa nimekuwa mnaniona naomba ridhaa kwenu nikifika Bungeni nikawapeleke kero zeni ila na Kutumia kipato Changu kushughulikia baadhi ya kero ninazoweza ikiwemo kuwanunulia gari la kubebea maiti kutoka Hospitali Kata zote 6 “Amesema Yusufu
Hata hivyo Yusufu Amebainisha kuwa Suala la Changamoto ya Maji ya Mvua kukosa miundombinu na Kutuama kukaa muda mrefu anakwenda kushughulikia kwa Kujenga Miundombinu ya Maji ili Kadhia hiyo iishe mara moja.
Aidha Mgombea huyo amewasisitiza Wananchi kuachana na Maneno yanayoenea kuwa Uchaguzi hakuna hao wote wanaozungumza hawana Sera wamekosa hoja majukwaani pia anatambua wengine ni wale Wanachama wa CCM ambao ni ndumilakuwili wanajiita CCM ” B” Octoba 29 Mwaka huu wajitokeze kupiga Kura Kiongozi wanaoona atakwenda kuwaletea Maendeleo.


