Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema kuwa raia yeyote ambaye hatampigia kura baba yake katika uchaguzi mkuu ujao, atafukuzwa nchini humo.

Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema kuwa raia yeyote ambaye hatampigia kura baba yake katika uchaguzi mkuu ujao, atafukuzwa nchini humo.

Nchi hiyo ya Afrika mashariki inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Januari mwaka ujao, na kumekuwa na ongezeko la msako dhidi ya wapinzani katika miezi ya karibuni.

Kaneiuragaba ambaye ni mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni pia amesema atawapiga marufuku wanawake jeshini kuvaa suruali.

Afisa huyo wa jeshi anayesifika sana kwa kuandika ujumbe wenye utata kwenye mtandao wa X, mapema mwezi huu, alidai kuwa alimkamata na kumtesa mlinzi wa kiongozi wa upinzani Bobi Wine, Eddie Mutwe, ambaye baadaye alionekana mahakamani bila alama zozote za kuteswa kwa mujibu wa Waziri wa Sheria Norbert Mao.