Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuwa kutakuwa na kukosekana kwa huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Morogoro na Tanga kuanzia Julai 9 hadi Julai 14, 2026, kupisha utekelezaji wa kazi za uvutaji waya (stringing) katika Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma.