Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa {Kulia}akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {katikati}pamoja na Mratibu wa Tigo Fiesta 2918 , Pancras Mayalla almaarufu Askofu TZA katika Mkutano na waandishi wa habari kueleza maandalizi ya tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika uwanja wa Nang’wanda Jumapili hii pamoja na ofa mbali mbali za kampuni ya Tigo katika msimu huu ikiwemo mfumo wa malipo kwa wakulima wa korosho kupitia huduma za Tigo Pesa.

.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {Katikati} akiongea na waandishi wa Habari {Hawapo Pichani} kuhusiana na fursa mbalimbali za biashara zinatazopatika katika mkoa huo kutokana na ujio wa tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ya wiki katika viwanja vya Nangwanda Sijaona. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa na Mratibu wa Tamasha la Tigo Fiesta, Pancras Mayalla {almaarufu Askofu TZA}.

MTWARA KUVUNA VIBE KAMA LOTE MSIMU HUU WA TIGO FIESTA 2018
Wateja wa Tigo kupata faida mara tatu kupitia promosheni za kusisimua

Mtwara, Oktoba 13, 2018 – Huku msimu wa mavuno ya korosho ukiwa umewadia katika mikoa
ya nyanda za juu kusini, wakaazi wa Mtwara na viunga vyake wanajiandaa kuvuna vibe kama
lote kutoka kwa mastaa wa muziki wa bongo flava katika msimu unaoendelea wa Tigo Fiesta
2018 – Vibe Kama Lote.
Waandaaji Clouds Media Group, kupitia Katibu Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi, Gardner
Habash amewaalika wakaazi wa Mtwara waje kupumzika baada ya shughuli ngumu za kuvuna
korosho kwa kusikiliza 100% vibe za nyumbani.
‘Kwa wafanya biashara, msimu waTigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ni fursa ya kujiongezea
kipato kwa kutoa huduma za usafiri, malazi, vinywaji na chakula na huduma nyingenezo
zinazohitajika na maelefu ya mashabiki watakaojitokeza kushuhudia tamasha hili,’ Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byanakwa alisema.
Kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota, wasanii wanaochipuka kutoka Mtwara
watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao, na wale watakaofanya vizuri watapewa fursa ya
kutumbuiza katika tamasha kuu la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linalotarajiwa kurindima
siku ya Jumapili tarehe 14 Oktoba katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa
vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote
itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo
Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa
4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH
milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo

2 | Page
Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno
MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz .
Watakaoshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and
Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo
ya wapenzi wa muziki mjini Iringa. Wengine ni wasanii a bongo flava Mesen Selekta na Foby,
wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.
TIketi za Tigo Fiesta 2018 – Mtwara zinapatikana kwa bei punguzo ya TSH 5,000 kupitia Tigo
Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua
namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika cha TSH 5,000 kwenda namba ya Tigo
Fiesta 78888888.

Tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote tayari limezuru mikoa ya Morogoro,
Sumbawanga na Iringa, na linatarajiwa kutembelea mikoa ya Singida, Songea, Moshi, Tanga,
Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku fainali ikiwa Dar es Salaam.

Please follow and like us:
Pin Share