Na Cresensia Kapinga, JakhuriMedia, Namtumbo.

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Ngolo Malenya amesema kuwa Mwenge wa Uhuru unaokimbizwa katika Wilaya hiyo utakagua,utaweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo 10 yenye thamani ya sh. Bilioni 2.5

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru kutoka Wilaya ya Tunduru alisema kuwa mwenge huo ukiwa Wilayani Namtumbo utaweka jiwe la msingi kwenye mradi wa barabara ,Mradi wa kituo cha mafuta,mradi wa bweni Veta, ugawaji wa vifaa kwa watu wenye mahitaji maalumu.

Ameitaja miradi mingine kukagua shughuli za lishe, kuzindua klabu ya kupinga Rushwa, kutembelea mradi wa uhifadhi wa mazingira Luegu, pamoja na kuzindua kisima kilichoboreshwa Kijiji Ruvuma.

Hata hivyo Meneja wa TARURA Wilaya ya Namtumbo Mhandisi Fabiani Lugalaba amesema kuwa ujenzi wa barabara za lami Namtumbo mjini zenye urefu wa k.m 1.6 umetekelezwa kupitia fedha za mfuko wa barabara na utekelezaji wake ulianza Disemba 2022 na kukamilika Juni 2023 ambapo kwa sasa mkandarasi yupo katika muda wa matazamio.