Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Maswa
Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 watua Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, ambapo utatembelea jumla ya miradi ipatayo 7 itakayogharimu jumla ya sh.bil.2.7, kwa mzungukio wa umbali wa km.147.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt.Vicent Anney wakati akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anamringi Macha mbele ya kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi katika eneo la makabidhiano ya mwenge huo Kijiji cha Njiapanda Kata ya Kisanga.

Amesema mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Maswa utafanya kazi ya kuzindua miradi kadhaa, kuweka mawe ya msingi miradi mitatu na kuzindua miradi miwili huku kuona na kukagua ikiwa ni miradi miwilii yote ikiwa na thamani ya sh.bil.2.7.
” Ndugu kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi, mwenge ukiwa hapa Wilaya ya Maswa utatembelea, kukagua miradi 7, kuzindua miradi 2, kuweka mawe ya ,singing miradi 3 na kuona na kukagua miradi 2″ amesema Dkt. Anney.
Aidha Mkuu huyo amesema kati ya sh.bil.2.7 Serikali Kuu imevhangia sh.2.63, Halmashauri imevhangia sh.mil.112, huku wananchi nao wakiwa wamechangia jumla ya sh.mil.5 katika shughuli mbalimbali za miradi ya Maendeleo inayopitiwa na Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025.

Akielezea miradi itakayopitiwa na Mwenge wa uhuru Kitaifa 2025 katika wilaya ya Maswa Dkt.Anney amesema ni pamoja na kukagua na kuweka jiwe la Msingi Mradi wa ujenzi wa yumba viwili vya madarasa, Ofisi ya walimu, pamoja na matundu ya vyoo katika shule ya Msingi Funika.
Miradi mingine itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kutembelea na kukagua miradi wa shughuli za kikundi Cha Vijana cha Maswa Sign, Mradi wa nne ni kuzinduamradi wa ujenzi wa majengo yanayotumika kuboresha huduma ya afya Kwa wananchi wa Wilaya ya Maswa.

” Mradi wa Tano ni mwenge utaweka jiwe la Msingi Mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa idara, Mradi wa sita Mwenge utazindua Mradi wa daraja la Malita pamoja na kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Saba wa Maji katika vijiji vya Buyubi, Dodoma na Ikungulyasubi.
Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 umetokea Mkoa wa Shinyanga na kuingia Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu ukiwa umefikisha jumla ya Mikoa 22.

