Na Jovina Massano, JamhuriMedia, Musoma

MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Wilaya ya Musoma Mkoani Mara Otaigo Mnanka aliejiunga na Chama Cha Ukombozi wa Umma ( CHAUMA)nafasi yake yapata mrithi.

Mrithi huyo amepatikana June 8,2025 mara baada Baraza hilo kufanya uchaguzi uliomuibua George Steven Kaunga kuwa Mwenyekiti mpya wa baraza hilo uliofanyika katika ofisi za Chama zilizopo Kata ya Kigera Manispaa ya Musoma.

Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Mara ambae pia ndie aliekuwa msimamizi wa uchaguzi huo Alphonce Machira amesema kutokana na nafasi hiyo kuwa wazi kwa mujibu wa katiba ya baraza nafasi ilitolewa kwa vijana alie na sifa kuomba ndipo wakajitokeza wagombea wawili.

“Wagombea walioomba kujaza nafasi hiyo ni wawili Isack Maulid na George Steven Kaunga mara baada ya kupokea maombi yao Isack Maulid aliamua kujiondoa na kumwacha George Steven Kaunga kwa mujibu wa katiba na utaratibu uchaguzi ukaendelea kwa kupiga kura za ndio au hapana na kuwezesha wajumbe kumpa kura za ndio”, amesema Machira.

Ameeleza wajumbe halali wapigakura ni viongozi wa majimbo mawili Jimbo la Musoma mjini na Jimbo la Musoma vijijini Idadi yao ni 9 ,kura za ndio 8 hapana 1.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa uchaguzi huo Hamad Nyasebwa ambae ni Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Musoma mjini amewaeleza vijana kuendelea kuunga mkono agenda ya No Reform No Election na kushirikiana na viongozi waliowaamini na kuwapa ridhaa.

“Tutashiriki uchaguzi endapo mabadiliko ya Katiba ya uchaguzi yatafanyika, BAVICHA jimbo la Musoma tunaungana na viongozi wetu katika safari ya kudai mabadiliko”,amesema Hamad.

Kwa upande wake mshindi wa nafasi hiyo George Steven Kaunga amewaomba viongozi wa Chama pamoja na wanachama na kushirikiana kwa miongozo,kanuni na Sera za chama ili kusimama imara.

Walioshiriki uchaguzi huo ni pamoja na Hamad Nyasebwa ambae ni Mwenyekiti wa Jimbo la Musoma mjini, Felix Changwe, Happness Kaunya,Joseph Charles, Baraka Masatu, Bahati Murwanga, Alphonce Machira,Isack Maulid, na George Steven Kaunga.