Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Nape Moses Nnauye amewataka wagombea wa nafasi ya mbalimbali kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanya kampeni zenye tija na kuchochea maendeleo.

Akizungumza leo Novemba 20 2024 mjini Sumbawanga Nape Moses Nnauye amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ni tofauti na 2019.

Amesema chama Cha Mapinduzi CCM kimejipanga ili kuhakikisha kinashika dola kwa kishindo kwa kufanya kampeni kwa lengo la kunadi sera zao.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Aesh Khalifan Hilary amesema kuwa Kila mwananchi ana wajibu na haki ya kumchagua kiongozi anayemtaka.

Katika mitaa yote 165 ,vijiji 339 na vitongoji 1816 chama hicho kimewasimamisha wagombea wote pamoja na wajumbe wake.

Mwenyekiti wa CCM Silaf Maufi amesema chama kipo imara na wana imani kubwa kuwa watashinda kwa kishindo.

Maufi amevitaka pia vyama vya upinzani kufanya kampeni zenye kuleta tija na maslahi kwa jamii na sio kutumia nguvu kubwa kwenye kampeni kufanya vurugu.

Akiongea kwa nyakati tofauti Nape amewataka wanachama na wananchi kusikiliza kampeni na kupima kama wanaweza na tarehe 27 kufanya maamuzi ya kupiga kura.

Amesema walifanya mchakato wa kuwapata wagombea kwa mfumo wa kura za maoni na wakapatikana wagombea watakaopigiwa kura na kwa kuwa ndio wameaminiwa na wananchi .

“Tunajiamini tumesimama imara kuhakikisha Tunashinda kwani yapo mambo tunayojivunia yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya mwenyekiti wake Dkt Samia Suluhu Hassan”.Nape Alifafanua zaidi

Baadhi ya wananchi wa Sumbawanga akiwemo Jackson Matofali na Suzan Ally wamesema kuwa ili uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 uwe huru na haki ni lazima vyama vya siasa vinadi sera zao na sio kutumia lugha chafu na kuona kama wanaonewa.

Naye mgombea nafasi ya mwenyekiti katika mtaa wa Mpasi Sospeter Twenya amesema wao watafanya kampeni za kistaarabu bila kuruhusu Hali yoyote ya vurugu.