Nassari amgaragaza Sioi kwa kura zaidi ya 7,000

HACKED BY NC TESLA GANS

Mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari, amembwaga mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sioi Sumari katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki. Kutangazwa kwa Nassari kuwa mshindi wa kiti hicho, kumeibua shamrashamra si Arumeru pekee, bali ndani ya nje ya nchi, hasa kwa wapenda mageuzi.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi, ametangaza kwamba Nassari amepata kura 32,972 wakati Sioi akipata kura 26,757. Mohamed Mohamed wa DP (77), Abdallah Mazengo wa AFP (kura 139), Khamis Kihemu wa NRA (35), Shaban Moyo (22), Charles Msuya wa UPDP (18) na Abraham Chipaka wa TLP (18).

Wapigakura walioandikishwa ni 127,455, lakini waliopiga kura ni 60,696. Kura 661 ziliharibika. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inaendelea kubangua bongo kujua sababu zinazowafanya watu wengi wasijitokeze kupiga kura.

Chadema wameongoza katika kata 14 kati ya 17 za Jimbo hilo. Kata ambazo imefanya vizuri zaidi ni Akheri ambako ni nyumbani kwa Sioi, Poli, Usa River, Mbuguni, Seela, Sing’isi, Nkoarua, Maji ya Chai, Kikwe, Maroroni, Nkoaranga, King’ori, Kikatiti, Ngarenanyuki na Songoro ambako ni nyumbani kwa Nassari.

Sioi amefanya vizuri katika kata za Makiba, Leguruki na Mkoandrua.

Katika miji mingi, baadhi ya wafuasi na wapenzi wa Chadema hawakulala. Walisubiri matokeo usiku kucha. Shamrashamra zilianza baada ya matokeo ya awali kuanza kutoka katika vituo vilivyo karibu na Mji Mdogo wa Usa River.

Wakati matokeo hayo yakitoka, wafuasi wa CCM waliendelea kujipa matumaini kwa kusema kwamba wangeweza kufanya vizuri vijijini kama ilivyo ada.

Hata hivyo, kadri matokeo yalivyoendelea kupatikana ndivyo CCM walivyoendelea kukata tamaa. Baadhi yao walianza kuondoka Usa River usiku huo huo kuelekea Dar es Salaam na katika miji mingine.

Chadema ilivyoigaraza CCM vituoni

Usa River Shule ya Msingi B CCM 37, Chadema 131. Ngarenanyuki Shule ya Msingi CCM 92, Chadema 95. Makumira CCM 48, Chadema 93. Kikatiti CCM 40, Chadema 119, Shule ya Msingi Ambuleni 3 CCM 58, Chadema 84.

Shule ya Msingi Usa 1 CCM 37, Chadema 116, Chuo cha Mifugo 2 CCM 46, Chadema 67, Chuo cha Ualimu 2 CCM 46, Chadema 101, Shule ya Msingi Leganga 2 CCM 27, Chadema 137, Shule ya Msingi Ndoombo CCM 83, Chadema 45. Moivaro Ofisi ya Kitongoji 3 CCM 45, Chadema 95, Songoro Shule ya Msingi 2 CCM 123, Chadema 98.

Ambureni Shule ya Msingi 2 CCM 47, Chadema 194, Ofisi ya Kata Mbuguni 1 CCM 99, Chadema 167, Shishton CCM 45, Chadema 208, Chama Ambureni A CCM 55, Chadema 130. Ambureni C CCM 42, Chadema 115, Ambureni D ,CCM 58, Chadema 118,

Ambureni E CCM 60 Chadema 111.

Ndoombo Shule ya Msingi CCM 85, Chadema 45, Ambureni Shule ya Msingi B CCM 47, Chadema 194, Ofisi ya Kijiji Nguluma 1 CCM 88, Chadema 94, Nguluma 2 CCM 164, Chadema 89, Songoro Shule ya Msingi CCM 123, Chadema 98. Shishton 1 CCM 52, Chadema 209, Ofisi ya Kijiji Nkoaresambo CCM 140, Chadema 113, Shule ya Msingi Ambureni CCM 58, Chadema 84.

Shule ya Msingi Savana 1  CCM 55, Chadema 60, Shule ya Msingi Savana 2 CCM 42, Chadema 49, Kyala Sing’isi 2, CCM 74, Chadema 174, Shule ya Msingi Mwelao 1 CCM 32, Chadema 141, Shule ya Msingi Mwelao 2 CCM 34, Chadema 149, Shule ya Msingi Mwelao 3 CCM 28, Chadema 139, Shule ya Msingi Mwelao 4 CCM 26, Chadema 126, Ngarenanyuki Shule ya Msingi 1 CCM 110, Chadema 120.

Sing’isi Kituo cha Kata CCM 74, Chadema 174, Maweni Shule ya Msingi B CCM 100, Chadema 88, Elimu Patandi 2 CCM 46, Chadema 101, Sinai Shule ya Msingi CCM 94, Chadema 30, Shule ya Msingi Miembeni CCM 102, Chadema 96, Mji Mwema A CCM 51, Chadema 144, Moivaro Kusini 1 CCM 34, Chadema 123, Kikwe Makumira Konshuma Kituo 3 CCM 42, Chadema 118, Kituo cha 4 CCM 40, Chadema 98.

Konshuma 1, CCM 42, Chadema 100, Ngarasero A Kiuo cha 4, CCM 51, Chadema 116, Ikwakilika CCM 92, Chadema 88, Mji Mwema A CCM 51, Chadema 144, Seela Shule ya Msingi, CCM 88, Chadema 108, Kimbenu Shule ya Msingi CCM 84, Chadema 116, Ngeku Shule ya Msingi 1 CCM 114, Chadema 118, Ngeku Shule ya Msingi 2 CCM 149, Chadema 95, na Seela 2 CCM 66, Chadema 131.

Chama cha Msingi Seela 1, CCM 91, Chadema 111, Shule ya Msingi Maleu CCM 99, Chadema 77, Shule ya Msingi Maleu 2 CCM 87, Chadema 100, Chama cha Msingi Mlala, CCM 94, Chadema 126, Nkoaranga Mahakamani CCM 49, Chadema 183, Moivaro Kusini 3 CCM 35, Chadema 95, Kikatiti Imbaseni Sokoni 1 CCM 316, Chadema 575, Maji ya Chai Zahanati 1 CCM 86, Chadema 139 na Maji ya Chai Zahanati 2, CCM 63, Chadema 134.

Shule ya Msingi Kikatiti CCM 128, Chadema 161,  Ofisi ya Kitongoji Mlimani CCM 78, Chadema 89, Songoro 2 CCM 110, Chadema 99, Kwaogoro 1 CCM 110, Chadema 104, Kwaogoro 2 CCM 83, Chadema 71, Kwaogoro 3 CCM 93, Chadema 86, Kwaogoro 4 CCM 80, Chadema 76.

Ofisi ya Kijiji Karangai 1 CCM 87, Chadema 100, Shule ya Msingi Moivaro 3 CCM 28, Chadema 139, Makumira Consumers CCM 50, Chadema 92, Nasura Shule ya Msingi 1 CCM 77, Chadema 79, Kituo 2 CCM 74, Chadema 91, Songoro Shule ya Msingi 3 CCM 110, Chadema 86.

Ofisi ya Kijiji Ndumae CCM 88, Chadema 94, Ngarasero 4 CCM 55, Chadema 118, Moivaro Kusini 2 CCM 30, Chadema 95, Ofisi ya Kitongoji Kisambare 3 CCM 60, Chadema 117, Kituo cha 2, CCM 58, Chadema 113 na kituo cha 5, CCM 50, Chadema 110,  Ngaresero A 1, CCM 140, Chadema 113, Shule ya msingi Imbaseni 3, CCM 58, Chadema 84, Ofisi ya kata Sing’isi 2, CCM 74, Chadema 174, Maweni Shule ya msingi B, CCM 100,  Chadema 88.

Kata ya Nkoanrua: Shule ya msingi Moivaro II CCM 28, Chadema 139, Moivaro ofisi ya kijiji III 45, Chadema 95, Moivaro Kusini I CCM 34, Chadema 123, Moivaro Kusini II CCM 30, Chadema 95 na Moivaro III CCM 35 na Chadema 95.

Kata ya Akheri: Chuo cha mifugo II CCM 46, Chadema 67, Chuo cha Ualimu Patandi II CCM 46, Chadema 101 na Akheri ofisi ya kijiji I CCM 88 na Chadema 94.

Matokeo mengine ni pamoja na Kituo cha Ushirika Ngyani A, Kata ya Nkoaranga, Chadema 168, CCM 102, Kituo Ushirika Ngyani B, Chadema 159, CCM 88. Moivaro Shule ya Msingi 1, CCM 34, Chadema 149, kituo namba 2, CCM 26, Chadema 126.

Kituo cha Uraki CCM 28, Chadema 56, Kata ya Kikwe kituo cha 1, Chadema 104, CCM142, Kituo B, Chadema 109 CCM 109, Kituo cha Miembeni Chadema 92, CCM 108, Chuo cha Patandi 1, CCM 42, Chadema 86, Ktuo cha 2, CCM46, Chadema 101 na kituo cha 3, CCM 47, Chadema 100.

Kata ya Makiba kituo cha Majengo, Chadema 96, CCM 103, kituo cha pili Chadema 339, CCM 365, kituo cha Patanumbe, Chadema 138, CCM 100, Kituo cha Zahanati, Chadema 61, CCM 67, Kituo cha Shule ya Msingi, Chadema 105, CCM 97.

Vituo vya kata ya Nkoaranga, Nkoaranga Barazani1, CCM 49, Chadema 183, Nkoaranga Barazani B, Chadema 169, CCM 50. Kituo cha Ofisi ya Kijiji Nkoaranga, CCM 97, Chadema 360 na vyama vingine zero.

Kata ya Mbuguni kituo cha Shule ya Msingi Msitu wa Mbogo, CCM 87, Chadema 68, Kituo cha Msitu wa Mbogo, CCM 76, Chadema 80.

Kituo cha kwanza Kata ya Kingori, AFP 1, CCM 117, Chadema 116, DP 1.

Matokeo kituo shule ya msingi Poli1, CCM 70, Chadema 85, DP 0, NRA 0, SAU 0, TLP 0, UPDP 0. Kituo cha pili, CCM 66, Chadema 85,  Kituo cha Leganga A, Chadema 142, CCM 26, AFP 1, Kituo Leganga B, Chadema 131, CCM 27.

Kituo cha Yumbeni 1, CCM 63, Chadema 59, kituo cha 2, CCM 64, Chadema 65, Kata ya Mbuguni Msufini Kijiji cha Kikuletwa, CCM 72, Chadema 131, Kituo cha Ofisi ya Kata Mbuguni, 3, CCM 107, Chadema 125 na  DP 1, Kituo cha Kampuni, Kijiji cha Msitu wa Mbogo, CCM 39, Chadema 22. Shule ya Msingi Mikungani Kata ya Mbuguni 1, CCM 52, Chadema 150, UPDP 1, namba 2, CCM 52, Chadema 106, Kituo cha 3, CCM 64, Chadema 111.

Kituo cha Nkoasenga kata ya Leguruki, CCM 132, Chandema, 108, Kituo cha 2, CCM 139, Chadema 185, Kituo cha 3, CCM 138, Chadema 94, AFP 2; Kituo cha 1, CCM 53, Chadema 130, Kituo namba 2, CCM 68, Chadema 108 na AFP 2, Kituo cha 3, CCM 42, Chadema 115, Kituo namba 4, CCM 58, Chadema 118 na kituo cha 5, CCM 60, Chadema 105 na AFP 1.

Ofisi ya Mtendaji Mjimwema kituo cha 2, Chadema 141, CCM 33, Kituo cha 3, Chadema 125, CCM 35, Kituo cha 4, Chadema 126 na CCM 35.

Kituo Poli Barazani, AFP 1, CCM 108 Chadema 136, Shule ya Msingi Msitu wa Mbogo A, CCM 76, Chadema 80, kituo B, CCM 83, Chadema 68, Ofisi ya Kata, Maji ya Chai 1, AFP 2, CCM 85, Chadema 132 na TLP 1, kituo 2, AFP 1, CCM 58, Chadema 135, kituo namba tatu, CCM 75, Chadema 125, DP 1, Kituo cha Zahanati 1, AFP 1, CCM 86, Chadema 139.

Kituo namba mbili AFP 1, CCM 63, Chadema 134, DP 1, Kituo shule msingi Imbaseni1, CCM 58, Chadema 84, Kituo 2, CCM 42, Chadema 96, Kituo namba tatu, AFP 1, CCM  51, Chadema 94, Matokeo kituo cha Nkwambiaa1, CCM 39, Chadema 150, kituo cha 2, CCM 45, Chadema 150, kituo 3, CCM 43, Chadema 154.

Kituo namba moja Kata ya Lenguruki mjini, kituo namba moja, CCM139, Chadema 86, kituo cha 2, CCM 139, Chadema 91, Kituo cha 3, CCM 16, Chadema 76, AFP1, NRA 1.

Kata ya Makiba, Shule ya Msingi Patanumbe, CCM 100, Chadema 138, kituo cha pili, CCM 97, Chadema 105, Zhanati ya Meta, CCM 67, Chadema 61 na Ofisi ya Kata Makiba, CCM 369 Chadema  339, Kituo Chama cha msingi poli 1, CCM 126, Chadema 152, DP 1 na NRA.

Nape aipongeza Chadema, akubali kushindwa, Nassari anena

CCM kupitia kwa Katibu wa Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, ametangaza kuyakubali matokeo hayo. Amempongeza Nassari na Chadema kwa kusema, “Nawapongeza, ndiyo sauti ya wana-Arumeru, tunaheshimu uamuzi wao, tunaheshimu matokeo.”

Kwa upande wake, Nassari, baada ya kutangazwa rasmi kuwa mshindi, aliahidi kushirikiana na wana-Arumeru Mashariki wote kujiletea maendeleo.

Amesema atashirikiana na wananchi wote bila kujali wapi alikopata kura nyingi au alikopata kura chache. “Tutawatendea haki wote bila kujali tofauti zilizokuwapo,” amesema Nassari.

Aidha, amelisifu Jeshi la Polisi kwa kusema limefanya kazi nzuri kwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru kwa wagombea wote.

Amemshukuru Mungu kwa kutumia kaulimbiu yake maarufu aliyoitumia muda wote wa kampeni ya, “Tumeanza na Mungu, Tutamaliza na Mungu”.

Mambo yalivyokuwa Arumeru

Arumeru Mashariki kulikuwa na vituo 327 vya kupigia kura. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilifanya marekebisho madogo katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Katika marekebisho hayo, NEC iliwaingiza wapiga kura 26 na kufanya idadi yao ifikie 127,455 kutoka watu 127,429 walioandikishwa kwenye Daftari hilo mwaka 2010.

Taarifa za marekebisho hayo zilitolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva. Akawatoa hofu wananchi kwa kusema marekebisho hayo ni halali.

Mwanzo wa kampeni

Kampeni za CCM zilizinduliwa Machi 12, mwaka huu na Rais mstaafu Benjamin Mkapa. Kwa Chadema, zilizinduliwa Machi 17 na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Vyama vyote vilizindua kampeni zake katika eneo la Mji Mdogo wa Usa River.

Kama ilivyokuwa Igunga, kiongozi wa kampeni za CCM Arumeru Mashariki alikuwa Katibu wake wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Mchemba. Chadema kampeni zake ziliongozwa na Mbunge wa Karatu, Mchungaji Yohana Natse, huku akisaidiwa na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere. Nassari na Sioi walifikia hatua hiyo baada ya kuruka viunzi vya uteuzi. Nassari alipita baada ya kupata ushindi wa kishindo wa kura 805, huku akiwaacha wagombea wenzake watano wakigawana kura 83 zilizosalia kati ya kura 888 zilizopigwa.

Sioi alilazimika kufanya kampeni na kushiriki kura za maoni mara mbili, baada ya ushindi wake wa kura 361 alizopata kwenye kura za maoni Februari 20, mwaka huu kutoridhiwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM. Kura zikapigwa upya kwa kumshindanisha na William Sarakikya.

Kwenye duru ya pili alipata kura 761 kati ya kura halali 1,122 zilizopigwa. Mpinzani wake alipata kura 361.

Sioi amemuoa binti wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, iliyowafanya wengi waamini kuwa ana nguvu za kisiasa kutoka kwa kiongozi huyo.

Sioi alitaka kuchukua kiti kilichoachwa na marehemu baba yake, Jaremiah Sumari, aliyefariki dunia mapema mwaka huu. Anajivunia rekodi ya kura 34, 661 alizopata baba yake mwaka 2010. Katika uchaguzi huo, Nassari alipata kura 19,123.

Kampeni za Arumeru Mashariki zilitawaliwa na vijembe na kuchafuana. Kwa mfano, Chadema walikuwa wakivumisha kwamba Sioi ametoga masikio, jambo ambalo si la kweli.

Wakati Chadema wakisema hivyo, kwa upande wa CCM wao walidai kwamba kitendo chao cha kuomba wachangiwe fedha kwenye kampeni kinatokana na Serikali ya Uingereza kuwanyima misaada baada ya kushindwa kuingia madarakani mwaka 2010.

CCM, wakiongozwa na Mchemba, wamekuwa wakisema kwamba endapo Chadema wangeshinda Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 wangelazimika kutekeleza sera ya wanaume kuoana.

Aidha, Mbunge wa Bunda, Steven Wasira, alikuwa akiwaeleza wananchi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa, aliiba fedha za ujio wa Papa Yohane Paul II hapa nchini mwanzoni mwa miaka ya 1990. Hata hivyo, Kanisa Katoliki lilikanusha madai hayo.

Pamoja na kuchafuana huko, funga kazi ya yote ikawa mvutano mkali wa kauli uliosababishwa na Mzee Mkapa kwamba Vincent Nyerere si mwanafamilia katika ukoo wa Nyerere.

Nyerere alijibu mapigo kwa kusema kwamba yeye ni mwanaukoo; kauli ambayo baadaye iliungwa mkono na Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage.

Nyerere alikwenda mbali zaidi kwa kumtaka Mkapa aeleze chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kilichotokea Oktoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mt Thomas London, Uingereza.

Tangu wakati huo kumekuwa na maneno mengi ya kumchafua Nyerere, yakiwamo ya kudai kwamba yeye ni mtoto wa nje ya ndoa katika familia ya Josephat Kiboko Nyerere. Hata hivyo, wanaoifahamu vema familia hiyo wanasema Nyerere ni mwanafamilia kwa nasaba.

Ukiacha vijembe, suala la sera lilipewa umuhimu na mgombea wa Chadema, Nassari ambaye mara zote alikuwa akiahidi kuwa endapo angechaguliwa atahakikisha anatatua kero kuu za ardhi, maji, barabara, huduma za afya na ukosefu wa ajira, hasa kwa vijana.

Nassari alionekana kuliteka jukwaa vema kuliko Sioi, na hiyo pengine inachangiwa na uzoefu alioupata kwenye uchaguzi wa mwaka 2010. Wakati Nassari alikuwa akihutubia kwa zaidi ya dakika 30, Sioi alitumia dakika zisizozidi 10.

Chadema yakandamiza udiwani Mwanza, Songea, Mbeya

Katika hatua nyingine, Chadema imeshinda udiwani katika miji ya Songea, Mbeya na Mwanza.

Katika Kata ya Kirumba mkoani  Mwanza, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Aloyce Mkono, amemtangaza mgombea wa Chadema, Danny Kahungu kuwa mshindi. Amepata kura 2,938 dhidi ya mgombea wa CCM, Jackson Masamaki aliyepata kura 2,131.

Haji Issa wa CUF amepata kura 184, Kasala Muhana wa UDP amepata kura saba na Athuman Jumanne wa NCCR -Mageuzi hakupata kura.