Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

Zama mpya ya huduma za kibenki imejili nchini baada ya Benki ya NMB jana kuzindua suluhisho ya kisasa inayomwezesha mteja kufungua akaunti kidijitali na kuanza kuitumia ndani ya dakika mbili tu.

Hatua hiyo kubwa inaongeza msukumo mpya katika jitihada za taifa za ujumuishwaji wa kifedha na upatikaji kiurahisi wa huduma za kidijitali za fedha.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Wareja Binafsi na Biashara, Bw Filbert Mponzi, sifa kubwa ya suluhisho la NMB Pesa Akaunti ni kuwa na mchakato mfupi wa kufungua akaunti mpya.

“Hii ni suluhisho yakusaidia kutatua changamoto za kifedha ambayo si tu ni akaunti inafunguliwa hapo hapo mteja alipo lakini pia ni nafuu kwasababu haina gharama nyingi kama ada za mwezi,”amesema Bw Mponzi.

Pia aliiambia hadhara iliyoshuhudia kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam kuwapindi usajili wa mteja mpya unapokamilika, akaunti yake itafunguliwa mara moja na kuanza kutumika moja kwa moja wakati huo ikiruhusu upatikanaji wa huduma zote za msingi kama ile ya NMB Mkononi.

Moja ya malengo yake makubwa ikiwa ni kuwakwamua Watanzania walio nje ya mfumo rasmi wa kibenki, NMB imeitambulisha sokoni huduma hiyo ya kufungua akauanti kidijitali kwa kasi zaidi nchini kwenye stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Magufuli Bus Terminal.

Mponzi alibwambia ngeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Amos Makala, kuwa ufunguaji huo mpya wa akaunti unafanyika mahala popote na hauhusishi kabisa karatasi ya aina yoyote na mfuguaji haitaji kwenda wala kufika katika matawi yao 228 yaliyotapakaa nchi nzima.

Jambo hilo limemfurahisha sana kiongozi huyo wa serikali ambaye kwenye hotuba yake aliesma hii sasa ni fursa kwa Watanzania wote kuwa na akaunti ya benki. Ufunguaji huo wa akaunti unafanyika kwa msaada wa wafanyakazi wa mauzo wa benki hiyo kwa njia ya simu za mkononi za aina zote.

Mponzi amesema huduma hiyo itakuwa ya muhimu sana hasa katika maeneo ambayo upatikanaji wa huduma za kifedha bado ni mdogo au haupo kabisa na wenye akaunti za benki ni wachache sana. Kwa sasa NMB inazo akaunti zaidi ya milioni tano na kila ziku zaidi ya 3,000 zinafunguliwa.

*Sote ni mashuhuda kuwa ulimwengu sasa unaelekea kuwa wakidigitali kwa karibia kila jambo, na kwa hilo Benki ya NMB imekuwa ikipambana kila mara kuibuka na masuluhisho ya kidigitali ambayo yatazidi kurahisisha utoaji huduma zetu lakini kuzifanya pia ziwe bora zaidi kwa wateja wetu,” amebainisha.

By Jamhuri