Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Kibaha

Wafanyakazi wanawake (staff) kutoka NSSF Mkoa wa Pwani wamewatembelea na kuwaona wazee wa kata ya Tumbi na kuwatakia heri ya mfungo wa Ramadhan.

Pamoja na mambo mbalimbali wazee waliomba wawe wanakumbukwa mara kwa mara kwa kuandaliwa programu za kuwakutanisha na ombi hili lilipokelewa na meneja wa NSSF.

Wazee na viongozi waliwashukuru NSSF kwa kuwapatia vitu vichache kwa ajili ya kumi la mwisho katika mfungo wa Ramadan .