Julius Nyerere: Tusipuuze misingi ya ujamaa

“Kama chama chetu kitapuuza misingi ya ujamaa, basi kitakuwa kinapuuza msingi mmoja muhimu wa amani na utulivu katika taifa hili. Tutavuruga amani maana tutakuwa tumeondoa matumaini ya kuleta maendeleo yanayoheshimu utu na usawa.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarange Nyerere.

Aung Suu Kyi: Saidia wengine mjifunze kujisaidia

“Kwa kuwasaidia wengine, mtajifunza namna ya kujisaidia wenyewe. Uhuru na demokrasia ni ndoto ambazo hamwezi kuziacha.”

Haya ni maneno ya Aung San Suu Kyi, Mwenyekiti wa chama cha upinzani, National League for Democracy (NLD) cha nchini Burma.

 

Kizza Besigye: Wasomi hawatusaidii chochote

“Nafikiri umefika wakati sasa kuorodhesha idadi ya wasomi wakiwamo maprofesa ambao ni sawa na janga katika nchi yetu [Uganda] ili kuwachukulia hatua kwa kuwa hawatusaidii chochote.”

Kauli hii ni ya kiongozi mstaafu wa chama cha FDC nchini Uganda, Dk. Kizza Besigye.

 

Papa Francis: Jamii isifumbie macho mateso

“Hakuna amani inayoweza kudumu, hakuna umoja na furaha katika jamii isiyojali, inayofumbia macho mateso.”

Haya yalinenwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, wakati wa ziara yake nchini Brazil, hivi karibuni.

Please follow and like us:
Pin Share