JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Profesa Mwamila ang’oka Chuo cha Mandela

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Profesa Burton Mwamila, amejiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi, JAMHURI linaripoti. Kujizulu kwa Profesa Mwamila, kumekuja siku chache baada ya vyombo vya ukaguzi…

Mchungaji amweka kinyumba kijana

Kituo cha Polisi cha Wazo Tegeta jijini Dar es Salaam katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kimeshutumiwa na wakazi wa eneo hilo kumlinda mhalifu anayedaiwa kumweka kinyumba mtoto wa kiume ambaye ni mwanafunzi (17). Kijana huyo (jina tunalo) anadaiwa kutekwa…

“TUEPUKE SUMU HIZI” (3)

“Mohamed Said, katika ukurasa wa 273 wa kitabu chake kuhusu Uislam anaandika kuwa Aprili, mwaka 1964, ujumbe mkubwa ukiongozwa na Sheikh Hassan Bin Amir, ukijumuisha akina Sheikh Said Omar Abdallah, Tewa Saidi Tewa, Katibu wa EAMWS – Abdul Aziz Khaki…

Tujitahidi Dodoma iwe ‘jiji’ badala ya ‘zizi’

Wapo ambao hadi leo hawajamwelewa Rais Dk. John Magufuli, na staili yake ya uongozi. Wamekuwa hawamwelewi kwa sababu ya mazoea. Hakuna dalili ya kumwelewa haraka leo au kesho! Lililo la muhimu ni kwamba muda utafika tu – watamwelewa. Baada ya…

Yah: Kilimo kwanza liwe ajenda ya kitaifa

Nianze waraka wangu kwa kuwapongeza viongozi wote ambao wanafanya kazi kwa msukumo wa kuleta mabadiliko ya kweli katika maendeleo ya taifa hili, mabadiliko ambayo lengo kuu ni kumuinua Mtanzania huyu maskini kwa kipindi kirefu awe na ahueni  ya maisha. Zamani …

Mangula, Mutungi na Safari kutaneni

Wazaramo wana misemo mingi katika lugha yao. Kati ya hiyo ni msemo usemao “Wose tozenga ing’anda imwe, habali tugombele lumango?” Katika tafasii sahihi ya Kiswahili “Wote tunajenga nyumba moja, kwa nini tugombee fito?” Nyumba ninayo kusudia kuizungumzia ni nchi yetu…