Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Tido Mhando (kushoto), amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar leo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa TBC.

Tido ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka ambapo moja ya mashtaka hayo ni uhujumu uchumi na kuisababishia TBC hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 887.

Tido alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Kwa kipindi cha miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya utangazaji wa radio ambapo alianza Utangazaji mwaka 1969 akiwa Radio Tanzania Dar es Salaam, (RTD), baadaye akafanya kazi Kenya, halafu Uingereza na hatimaye akarejea tena RTD kabla ya kuwa TBC.

Kwa sasa Tido Muhando ni Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media.

By Jamhuri