Latest Posts
Walinzi GGM watuhumiwa kwa ujambazi
Kashfa nzito imeukumba Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), baada ya baadhi ya walinzi wake kudaiwa kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha.
Imedaiwa kuwa walinzi hao wanapomaliza kufanya matukio hayo yakiwamo ya utekaji na uporaji, fedha zinazopatikana huzitumia kuwaziba midomo baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola wasiwafikishe katika mkono wa sheria.
Nyalandu apangua ‘amri’ ya Nyerere
*Aagiza wataalamu wafungue mpaka wa Bologonja
*Watalii kutoka Kenya wataingia kiulaini Serengeti
*Watafaidi vivutio, kisha fedha zote zitaishia Kenya
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameshakamilisha mipango ya kufungua mpaka wa Bologonja; jambo linalotajwa kuwa ni pigo kwa uchumi wa Taifa na kwa wadau wa tasnia ya utalii nchini.
Mpaka huo unaotenganisha Tanzania na Kenya, ulifungwa mwaka 1977 kwa amri ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi na kimazingira ya Taifa.
Taarifa zilizopatikana kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii zinasema tayari Nyalandu ameshawaagiza viongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na wengine katika Wizara yake, kuhakikisha mpaka huo unafunguliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Aloyce Nzuki, ambaye Nyalandu amemwondoa kwenye nafasi hiyo, anatajwa kuwa mmoja wa watu waliopinga mpango huo kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake. Upinzani huo unatajwa kuwa miongoni mwa sababu alizotumia Nyalandu kushinikiza Nzuki aondolewe.
Siri zavuja Bandari
Real Madrid kuivua ubingwa Bayern leo
Miamba minne ya soka barani Ulaya, wiki hii inajitupa tena katika viwanja viwili tofauti kucheza nusu fainali ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Miamba hiyo ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, vijana wa Pep Guardiola wa Bayern Munich,…
Biashara zinahitaji akili za kisasa
Wiki mbili zilizopita, nilipata wasaa wa kuongea kwa kirefu kwa njia ya simu na mjasiriamali kutoka mkoani Singida. Katika mazungumzo yetu mjasiriamali huyu wa miaka mingi alilalamika namna biashara zilivyobadilika nyakati hizi na namna ushindani unavyotishia mustakabali wake.
Mjasiriamali huyu alinipa mifano ya namna zamani alivyokuwa akipata faida kubwa katika bidhaa mbalimbali. Anaeleza, “Zamani nilikuwa nakwenda Dar es Salaam na kununua unga wa ngano kwenye mifuko ya kilo 50, nikija hapa Singida nikiuza kwa jumla ninapata faida ya hadi shilingi elfu tano. Leo hii mfuko wa unga wa kilo 50 huwezi amini, ninapata faida isiyozidi shilingi mia tano!
CCM inapohusishwa na kila kitu
Katika maisha ya jadi niliyoishi kijijini, kila kitu kilichotokea kilihusishwa na Mungu. Kama kuku hawakutaga mayai mengi kutokana na kutopewa chakula cha kutosha, watu walisema ni amri ya Mungu.
Kama mtu alikufa kwa ugonjwa kwa sababu ya kucheleweshwa kupelekwa hospitali, watu walisema ni amri ya Mungu. Na kama watoto walichezea moto ukaunguza nyumba, watu walisema ni amri ya Mungu.
- CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalishwa zaidi ya ajira 500
- Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi
- RC Ruvuma akabidhi magari 24 kwa Jeshi la Polisi
- Ridhiwani aahidi upatikanaji maji kwa asilimia 100, kaya 300,000 kufikiwa
- Mgombea urais CUF, Gombo aahidi wazee miaka 60 akiingia madarakani watalipwa posho kila mwezi
Habari mpya
- CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalishwa zaidi ya ajira 500
- Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi
- RC Ruvuma akabidhi magari 24 kwa Jeshi la Polisi
- Ridhiwani aahidi upatikanaji maji kwa asilimia 100, kaya 300,000 kufikiwa
- Mgombea urais CUF, Gombo aahidi wazee miaka 60 akiingia madarakani watalipwa posho kila mwezi
- Marekani yaharibu meli inayodaiwa kuwa ya dawa za kulevya ya Venezuela
- Israel yaanza operesheni ya ardhini Gaza City
- Dk Biteko amnadi Musukuma, asema amepigania maslahi ya wana-Geita
- Mama Salma: Njia pekee kuthamini kazi kubwa aliyofanya Dk Samia ni kumpa kura, Ridhiwan kiongozi mwenye dira
- Soma Gazeti la Jamhuri Septemba 16 – 22, 2025
- Kufufuliwa kwa reli ya TAZARA, ujenzi wa reli kusini utaleta mageuzi makubwa kiuchumi
- Trump asema yuko tayari kuiwekea vikwazo Urusi
- WHO: Chanjo ya Ebola imeanza kutolewa kusini mwa Kongo
- Luhaga Mpina aondolewa katika orodha ya wagombea urais 2025
- Mpina ajibu mapingamizi yake, amwekea pingamizi mgombea wa CCM Dk Samia