JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Dk. Remmy Ongala bado anakumbukwa

Siku hazigandi. Nathubutu kusema hivyo kwani Desemba 13, 2013 ndiyo siku ambayo nguli Ramadhan Mtoro Ongala ‘Dk, Remmy’ alitimiza miaka mitatu tangu aiage dunia. Dk. Remmy alifariki usiku wa kuamkia Jumatatu, Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam, baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya kisukari. Akawaacha wapenzi wake wa muziki wa dansi na Injili pia wananchi kwa ujumla katika dimbwi la majonzi yasiyosahaulika kutokana na tungo za nyimbo zake, ambazo hadi leo zinarindima katika vituo vingi vya redio hapa nchini na hata nje ya mipaka yetu.

Siri ya Mandela

*Alisahau viatu vyake vya kijeshi Tanzania, akafungwa

*Mufti Simba, Askofu Kilaini, Ruwa’ichi watoa tamko

*Profesa Baregu, Wangwe, Safari, Kiwanuka wanena

 

Kifo cha Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela “Madiba”, kimefichua siri nzito kuhusu harakati zake za ukombozi wa taifa hilo kutoka katika makucha ya serikali ya kibaguzi ya Wazungu.

M23 yawafika mazito

*UN waanza kutumia ndege zisizo na rubani kusaka masalia

*Zinatambua aliko mwenye bunduki, zilitumika Afghanistan

 

Baada ya Brigade Maalum ya Umoja wa Mataifa ikiongozwa na Jenerali wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwasambaratisha waasi wa M23 nchini DRC, Brigade hiyo imeanza kutumia ndege zisizokuwa na marubani (drones) kufanya ulinzi katika mji wa Goma, hali inayozidi kuwafukizia moshi waasi hao.

Jahazi Asilia: CCM, CUF wanahofu vivuli vyao

Chama cha Jahazi Asilia kimesema mtindo unaotumiwa na vyama vya CCM na CUF kubeba wanachama kwenda na kurudi kwenye mikutano ya hadhara hauvikisaidii vyama hivyo kujitambua na kupima kisiasa kama vinakubalika au la.

Dunia inalilia mawazo sahihi ya Mandela

Usiku wa Desemba 5, 2013 dunia ilipata habari mbaya. Nasema ilipata habari mbaya ambazo kimsingi zilitarajiwa, ndiyo maana sikutumia neno mshituko. Mzee wetu Nelson Madiba Mandela aliaga dunia.

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (9)

Katika sehemu ya nane, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema Rais ndiye aliyekiri kosa la Zanzibar kuingia katika OIC na pili ndiye aliyelazimika kukiri kule Dodoma kwamba utaratibu wa kushughulikia hoja ya Utanganyika ulikosewa lakini mawaziri wake mara zote mbili walitulia tu nakumuacha Rais ndiye akiri kosa na kubeba lawama. Ifuatayo ni sehemu ya kitabu cha Mwalimu Nyerere alichokiandika mwaka 1994 cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Endelea…

 

Katiba ya nchi yetu, na utaratibu tunaojaribu kujenga, vinataka kuwa katika hali kama hiyo, Mawaziri ndiyo wawajibike, na hivyo kumlinda Rais, si Rais awajibike, na kuwalinda Mawaziri wake, na tena  kwa kosa ambalo si lake. Watu walioshindwa uongozi Bungeni, hata tukafikishwa hapa tulipo leo, ni Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM.