Latest Posts
KONA YA AFYA
Sababu za kupungua nguvu za kiume -3
Homoni ya kiume iitwayo testestorone, ambayo hutolewa na korodani husimamia kazi ya uume kama vile kuleta msisimko, hamu ya tendo la ndoa, kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa.
Maswi: Gesi imeanza kuwatajirisha Mtwara
“Kazi ya kuunganisha na kusambaza mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam imefikia hatua ya kuridhisha. Kazi hiyo inafanywa na mashirika yenye uzoefu mkubwa kimataifa, ambayo ni Shirika la Teknolojia na Mendeleo ya Petroli la China (CPTDC), Kampuni ya Kutengeneza Mabomba ya China (CCP), Worley Parsons Limited na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Tayari mpaka sasa kilomita 142 kati ya 542 zimekamilika. Mradi huo unaotarajiwa kukamilika Desemba mwakani na utakuwa na mitambo ya kisasa.”
Yah: Mheshimiwa Kikwete: wananchi wanasema yatosha!
Salamu nyingi sana kama mchanga wa pwani zikufikie mahali popote ulipo, hofu na mashaka ni juu yako uliye mbali na upeo wa macho yangu, na baada ya salaam je hujambo.
Rais anasubiri nini kuifumua Wizara ya Elimu
kama tujuavyo imebaki miaka miwili Rais aliyepo madarakani Jakaya Mrisho Kikwete amalize muda wake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tayari tumemsikia Rais Kikwete akijivunia utendaji wake Amesema kwamba wale walioendelea kumsema vibaya kwamba chini ya uongozi wake Tanzania haikupata maendeleo wataoona aibu atakampomaliza muda wake. Atakuwa ameiacha Tanzania ikiwa na maendeleo yasiyo na kifani.
Mwarobaini hutibu mnyauko wa migomba
Mwarobaini ni mojawapo ya mimea maarufu yenye kinga dhidi ya wadudu waharibifu. Ndani yake kuna dawa inayoweza kutolewa kwa urahisi na kutayarishwa na kutumika kama dawa ya mimea ya kuulia wadudu.
Kinachonifanya nimpende Lowassa, hitimisho
Wakati naandaa makala niliyosema “Kinachonifanya nimpende Lowassa ni hiki” na kuichapisha katika gazeti hili la JAMHURI wiki iliyopita, hayakuwa mategemeo yangu kama makala hiyo ingeigusa jamii kwa kiasi nilichokishuhudia. Nimepigiwa simu nyingi mno, nimetumiwa ujumbe mfupi wa maandishi mwingi, na bado mpaka sasa naendelea kupokea simu na ujumbe!