Latest Posts
Je, wote tuwe wajasiriamali?
Nianze kwa kushukuru na kutambua mirejesho ya wasomaji wa safu hii ambao wanaongezeka kila wiki. Mirejesho mnayoniletea kwa ujumbe mfupi wa maandishi, kupiga simu na kuniandikia baruapepe ina thamani na umuhimu mkubwa sana katika kunogesha safu hii.
Serikali iwanusuru mabalozi wetu
Katika toleo la leo tumechapisha taarifa zenye kuonyesha kuwa hali ya kifedha ya Balozi za Tanzania nje ya nchi ni mbaya. Habari hizi zinaonyesha kuwa Balozi karibu zote zinakabiliwa na madeni, zimekatiwa huduma za simu, maji, umeme na mifumo ya…
Mahakama imekalia haki yangu miaka 16
Mhariri wa JAMHURI nimevutiwa kwa kiwango kikubwa baada ya kusoma toleo lenu Na 39 la Agosti 14-20, 2012 lililoongozwa na habari yenye kichwa kisemacho ‘Majaji Vihiyo Watajwa’. Mara tu niliposoma habari hii, nikaona ni vyema nifunge safari na kuja hapo ofisini kwako nieleze kilio changu. Wengi wa majaji waliotajwa wameshiriki kwa namna moja au nyingine kukandamiza haki yangu.
Bunge la sasa linaelekea wapi? (2)
Duniani kote upinzani huwa una tabia ya kuchokonoa upungufu wa hoja na kisha kuonyesha vipi maboresho yangekuja kama wao wangeongoza Serikali. Hii maana yake bungeni unakuwapo ukosoaji wa aina mbili.
Balozi za Tanzania aibu tupu
*Baadhi hawajalipwa mishahara miezi sita, zimeajiri Wakenya
*Ufaransa pango Sh milioni 720, wanatumia anwani ya Uganda
*Ofisi zinaporomoka, Kikwete asema Richmond imeiponza nchi
*Membe alia Serikali kukata bajeti yake ikabaki asilimia 44 tu
Sura na heshima ya Tanzania nje ya nchi inashuka kwa kasi kubwa, kutokana na Serikali kuzitelekeza balozi zake nje ya nchi.
Yapo mambo mengi ya aibu yanayowakumba mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi, kwani baadhi ya balozi zinashindwa kulipia huduma ya simu, maji, umeme na baadhi ya magari yanazimika na kuwashwa kwa kusukumwa kama ya uswahilini. Taarifa ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea balozi mbalimbali imeibua uozo wa ajabu.
Majaji maji shingoni
*Maelezo ya Jaji Ramadhani, Luanda moto
*Ripoti ya Ikulu nayo yataka waondolewe
*Lissu ataka wapime, kumshitaki Kikwete
*Amtaka Jaji Kiongozi Fakih Jundu ajiuzulu
Mhimili wa Mahakama umetikisika baada ya kuwapo ushahidi wa wazi kwamba Rais Jakaya Kikwete amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa kuwaongezea mikataba ya kazi baadhi ya majaji na kumpandisha cheo mwingine.