Latest Posts
Tuache kasumba ya kupuuza kila linalozungumzwa na Wapinzani
Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, amezungumza mambo mazito mno mwishoni mwa wiki. Sehemu ya hotuba yake tumeishapisha neno kwa neno ndani ya gazeti hili.
Ufisadi watikisa Bunge
*Unahusu kada wa CCM anayechimba urani
*Profesa Tibaijuka amtwika mzigo Jaji Werema
*Naibu Spika aagiza Waziri Muhongo ajiandae
*Sinema nzima imeibuliwa na Halima Mdee
Wafanyabiashara ndugu wanaodaiwa kubadili matumizi ya ardhi kutoka uwindaji wa kitalii na kuanza harakati za uchimbaji madini ya urani, wameibua mgongano mkubwa bungeni na serikalini. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amemwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, asaidie kupata utatuzi kashfa hiyo.
Kwa dhuluma hii nchi haitatulia
Ndugu msomaji, tazama picha iliyo katika ukurasa huu, kisha utafakari. Nimeitumia kama kielelezo halisi cha kutusaidia kuibua mjadala wa maana kuhusu hatima ya umasikini unaowaandama watoto wa masikini katika Taifa letu.
Hotuba ya Lissu iliyolitikisa Bunge, Serikali
*Atoboa siri majaji wengi ‘vihiyo’, washindwa kuandika hukumu
*Aeleza namna wakuu wa wilaya walivyoteuliwa kwa rushwa
*Yumo mwingine aliyehukumiwa kwa ubaguzi wa ukabila
Ifuatayo ni sehemu ya maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, kuhusu Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013. Lissu alitoa maoni haya na kwa kiasi fulani yaliibua mjadala mkali bungeni, huku Serikali ikitaka aondoe baadhi ya maneno, na yeye akakataa. Endelea…
UTEUZI WA MAJAJI
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua ukweli kwamba Rais Kikwete ameteua majaji wengi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kuliko marais wengine wote waliomtangulia kwa ujumla wao. Rekodi hii peke yake inaonyesha kwamba Rais anatambua umuhimu wa Mahakama Kuu kuwa na watendaji wa kutosha wa utoaji haki ili kutekeleza dira ya ‘haki kwa wote na kwa wakati.’
January Makamba amefanya jambo la kuigwa
Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba, ametangaza kuwa amejipanga kuongeza kasi ya maendeleo ya elimu katika jimbo hilo, kazi itakayofanyika kwa kupitia Shirika la Maendeleo Bumbuli (BDC) kuanzia mwaka huu.
Programu hiyo itagharimu Sh. milioni 40 ikijumuisha vivutio kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari; yote ikilenga kuongeza tija na umakini wa kujifunza na kusaidia juhudi zinazofanywa na serikali katika elimu.
Ardhi ya Tanzania inavyoporwa na matajiri matapeli
*Kambi ya Upinzani yaanika bungeni uozo wa kutisha
*Familia ya Chavda yavuna mabilioni na kutokomea
Hii ni sehemu ya hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee, aliyoitoa bungeni wiki iliyopita, akieleza namna ardhi ya Tanzania inavyohodhiwa na wafanyabiashara na matajiri matapeli…
MASHAMBA YALIYOBINAFSISHWA AMBAYO HAYAJAENDELEZWA
Mheshimiwa Spika, wakati akihitimisha bajeti ya ardhi mwaka jana, Waziri wa Ardhi aliliahidi Bunge lako Tukufu kwamba baada ya Bunge la bajeti wizara ingekwenda kufanya ukaguzi huru wa nani ametelekeza mashamba. Alisisitiza kwamba wawekezaji wote waliotelekeza mashamba “the honeymoon is over.”