JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Dk. Mwakyembe fahamu tumeshindwa reli, ndege makusudi

Wiki iliyopita Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe alisoma mipango lukuki katika bajeti ya Wizara ya Uchukuzi. Sitataja takwimu maana hizo kila awaye amezisikia. Sifurahi kutaja hata kiasi cha fedha zilizotengwa maana siku hizi namba zinatajwa bungeni, katika utekelezaji inakuwa sifuri.

Migogoro imeiua Simba msimu huu

Hatimaye Mashindano ya Ligi Kuu ya Vodaco Tanzania Bara yamemalizika huku Klabu ya Simba ikiambulia kushika nafasi ya tatu, huku mtani wao wa jadi, Yanga ikitwaa ubingwa wa ligi hiyo, ikifuatiwa Azam FC iliyoshika nafasi ya pili.

Wanawake ni injini ya ujasiriamali

  Wakati fulani nilikuwa nikisikiliza wimbo ulioimbwa na mwanamuziki nguli, Luck Dube, na ukatokea kunivutia sana kutokana na maudhui yake.   Ndani ya kibao hicho, Dube anaeleza namna wanawake wanavyopambana na maisha kupitia kujituma kuhakikisha familia zao zinastawi vizuri. Hata…

Mwalimu Nyerere na usawa katika jamii

 

Taifa letu kwa sasa linapita kwenye misukosuko ya udini, ukabila, ukanda na utegemezi. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hakusita kamwe kukemea kwa nguvu zote utengano huo, na kusisitiza nchi kujitegemea.

NUKUU ZA WIKI

Nyerere: Jeshi letu ni la Kizalendo

“Jeshi letu haliwezi kuwa Jeshi la mamluki, ni Jeshi la Kizalendo. Matumaini yangu ni kwamba Jeshi letu litaendelea kulinda na kutetea misingi mikuu ya Azimio la Arusha.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye pia ni mwasisi wa Azimio la Arusha.

Polisi wachunguze tuhuma hizi

Habari kubwa katika toleo la leo inahusu mtandao wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Liberatus Barlow. Ndani ya habari hiyo, gazeti hili la JAMHURI linamtaja mtuhumiwa Mohamed Edward Malele, Mkazi wa Kijiji cha Igoma, Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza anayekisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30 hadi 40 kuwa anashikiliwa na dola.