JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Katiba ya nchi siyo ya CCM

Mhariri JAMHURI,

Nachukukua nafasi hii kwanza kulipongeza Gazeti la JAMHURI kwa kujitolea kuweka wazi kuhusu dawa za kulevya na pia kuhusu  uwindaji haramu.

Chadema sasa wajiandaa kutumia nguvu Ukerewe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, kimetamba kwamba kitatumia nguvu ya umma kuishinikiza Mahakama imtoe rumande Mbunge Salvatory Machemli. Mahakama ya Wilaya iliamuru Mbunge wa Ukerewe apewe adhabu ya kwenda jela siku 14 kuanzia Novemba 6 hadi 20, mwaka huu, kutokana na kudharau amri iliyomtaka ahudhurie mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi namba 19/2013 inayomkabili.

Sababu za kupungua nguvu za kiume -2

Udumavu wa kufika kileleni: Huu ni upungufu wa nguvu za kiume. Ni hali ya kufika kileleni ambayo hutokea kwa polepole sana au kushindwa au kutokuwa na uwezo kabisa wa kufika kileleni kutokana na ukosefu wa shahawa. Ufikaji kileleni unaorudi: Huu…

Yah: Nimechoka na haki ya sheria!

Yah: Nimechoka na haki ya sheria!

Navuta shuka ambalo ni chakavu sana linaruhusu mbu waingie bila kipingamizi na kuning’ata, natumia dawa mseto kama tiba yangu kila wakati, sasa nimewazoea  mbu kiasi cha kutonifanya nishindwe kupata usingizi mzito.

Eneo la Shule ya Mwongozo Kinondoni kumegwa

Katika mambo mengi mazuri ambayo Serikali imeyafanya, hapana shaka ni kujenga uzio au kuta kuzunguka maeneo ya shule.

Kikwete: Kagame, Museveni, Kenyatta wamenishangaza

 

Asema wamevuja Mkataba, Itifaki ya Afrika Mashariki

Asisitiza Tanzania inaipenda Jumuiya, haitatoka kamwe

Aonya wasahau ardhi, ajira, kuharakisha shirikisho

Alhamishi wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza mambo manne ya msingi. Amezungumzia mchakato wa Katiba mpya, Operesheni Tokomeza,  ushiriki wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na hatima ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kutokana na umuhimu wa hotuba hii, na historia inayoweza kuwa imewekwa na hotuba hii katika siku za usoni, Gazeti JAMHURI limeamua kuchapisha hotuba hii neno kwa neno kama sehemu ya kuweka kumbukumbu na kuwapa fursa Watanzania, ambao hawakupata nafasi ya kuisikiliza hotuba hii, kuisoma na wao pia kuhifadhi kumbukumbu. Endelea…