Mhariri JAMHURI,

Nachukukua nafasi hii kwanza kulipongeza Gazeti la JAMHURI kwa kujitolea kuweka wazi kuhusu dawa za kulevya na pia kuhusu  uwindaji haramu.

Cha kusikitisha ni jinsi biashara ya dawa za kulevya inavyoendeshwa nchini. Na hivyo ndivyo uwindaji haramu unavyoendeshwa na watu maarufu kama vile wafanyakazi serikalini na wafanyabiashara maarufu nchini.

 

Kwa mantiki hii lengo langu hasa katika barua hii ni kuipongeza Tume ya Katiba mpya kwa kukusanya maoni ya Katiba mpya kutoka kwa wananchi wa Tanzania.

Na pia si vyema kuacha kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete, kwa kuwa makini na mchakato mzima wa Katiba Mpya.

Juu ya hayo, kupitia barua hii si jambo la amani kwa baadhi ya viongozi wa CCM kutaka kuifanya Katiba ya nchi  sawa na ile ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Baada ya kufuatilia kwa undani nikabaini ufisadi uliojikita katika Serikali ya CCM, ni chanzo cha kuwa na hofu ya kuwapo na Katiba itakayoungwa mkono na umma wa Kitanzania. Wanaotaka kuchakachua maoni ya wengi ni mafisadi.

 

Swali kuu ni je, kwa nini sehemu ndogo ya mafisadi inaiyumbisha Serikali ya CCM?

Nahitimisha barua hii nikiwa na matumaini ya kuwa maoni yangu kupitia barua hii, si maoni yangu tu bali ni wengi wanaokubaliana na kuunga mkono Katiba mpya iundwe kulingana na matakwa ya wengi.

Halitakuwa suala la busara kwa CCM kutaka kuonesha umma wa Kitanzania na umma wa nchi nyingine eti Katiba mpya inaundwa kwa misingi ya kupendelea upande wa vyama vya upinzani.

Tume ya Katiba mpya haijaundwa na vyama vya upinzani tu. Na Katiba ya nchi siyo ya chama kimoja cha (CCM).

Bwana na Bi. Isaya Majaliwa

C/o Kolandoto Hospitali,

Shinyanga.

By Jamhuri