Maafisa wengine 200 wa Polisi wa Kenya waliondoka Jumatatu usiku kuelekea Haiti, chini ya mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unaolenga kumaliza ghasia za magenge ya wahalifu katika taifa hilo la Caribbean.

Taarifa hii imetolea na maafisa wakuu wa polisi wa Kenya waliosema kuwa zoezi hilo litaendelea hadi kufikia idadi ya polisi 1,000. Kundi la kwanza la maafisa 400 waliwasili Haiti mwezi Juni.
Kwa miaka mingi Haiti imekuwa ikikabiliwa na uhalifu wa magenge wa watu wenye silaha ambayo kwa sasa yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu wa Port-au-Prince na pia barabara kuu katika nchi hiyo maskini ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa pia na misukosuko ya kisiasa.