JESHI la Polisi kanda Maalumya Dar es Salaam limekamata silaha mbalimbali zikiwemo bunduki, bastola na vifaa vingine vya kufanyia matukio ya uhalifu pamoja na watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya uhalifu ambao walikuwa wakijiandaa kutekeleleza matukio hayo.

 

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo limekamata silaha aina ya AK 47 na watuhumiwa wawili nyumbani kwa mzee Said Omary (62) baada ya kupata taarifa kuwa kuna wahalifu wanataka kufanya tukio la wizi wa kutumia silaha.

 

Aidha Polisi imewakamata watuhumiwa 2 wa wizi wa magari ambao baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na radio call, kadi 10 za benki mbalimbali, leseni za udereva, master keys 15 ambapo baada ya kuhojiwa walikiri kutekeleza matukio mbalimbali ua uhalifu huku wakionesha magari mawili na pikipiki moja vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi.

2552 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!