Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwan

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limekanusha kuhusika na tukio la ajali ya kugonga na kusababisha kifo cha Pendo Mugisa Mashauri (20), kilichotokea katika eneo la Kongowe, wilayani Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, amesema tukio hilo lilitokea Disemba 19, 2025 majira ya saa 2 usiku, huku kukiwa na taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii zikidai kuwa ajali hiyo ilihusisha gari la polisi, jambo ambalo amesema si la kweli.

Morcase aliwataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi halihusiki na ajali hiyo.

Alifafanua kuwa ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu ya Morogoroโ€“Dar es Salaam, ambapo gari lisilotambulika namba zake za usajili, likitokea upande wa Morogoro, lilimgonga mwanamke huyo na kumsababishia majeraha makubwa.

โ€œBaada ya ajali, wananchi walimkimbiza majeruhi katika Kituo cha Afya White Hope, Miembesaba, ambako alipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, ambako alifariki dunia tarehe 20 Disemba 2025,โ€ alisema Morcase.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo haikuripotiwa kwa wakati katika kituo chochote cha polisi, bali taarifa ilifikishwa tarehe 22 Disemba 2025 na shemeji wa marehemu aitwaye Kelvin Leonard.