Kesho Agosti 28,2025 kama ilivyotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kampeni za wagombea nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani zitaanza rasmi.

Jeshi la Polisi Tanzania, lingependa kuwajulisha wananchi na wadau wote kuwa, lipo tayari na limejiandaa vizuri ipasavyo kuhakikisha tunaendelea kuimarisha usalama wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wagombea na wafuasi wao na wananchi wote kwa ujumla, kukumbuka kuwa, jukumu la kudumisha Amani, Utulivu na Usalama ni letu sote kama Watanzania na kamwe asiwepo mmoja wetu  akawa chanzo cha kukiuka Sheria, Kanuni na Taratibu wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni ili kuepuka vurugu au uhalifu wa aina yeyote ile kutokea.

Pia tunatoa wito kila mmoja azingatie ratiba na muda wa kampeni aliopangiwa ili kuepuka mivutano, migongano, migogoro au uhalifu kutokea kwani hatutasita kumchukulia hatua kama sheria za nchi zinavyoelekeza.

Imetolewa na:

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi

Dodoma,Tanzania