Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania imeendelea kusimamia bandari za mwambao na maziwa makuu kwa kufanya uboreshaji ikiwemo kuongeza kina kikubwa ili kuweza kuruhusu Meli za Kisasa kuingia.

Akizungumza na jijini Dar es salaam Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema lengo la kufanya uboresha wa bandari hizo ili kusaidia meli kubwa za kisasa ziweze kuingie na sio kwenda kwenye bandari za nchi za jirani.

Profesa Mbarawa amesema kuwa amesema vipaumbele vya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23 vinakusudia kuhuisha uchumiwa nchi na kuwakomboa Watanzania wangazi zote

Amesema kuhusu upanuzi wa Bandari Dar es Salaam amesisitiza kuwa ujenzi wa gati namba 8-11 unaenda sambamba na upanuzi wa gati namba 1-2 katika Bandari ya Tanga ili kuziwezesha bandari hizo kufanya kazi kwa ufanisi.

‘Serikali pia itaendelea na upanuzi wa Bandariza Dar es Salaam na Tanga, Ujenzi wa Meli katika Ziwa Victoria na Tanganyika, upanuzi wa viwanja vya ndege nchini na ujenzi wa nyumba za viongozi na watumishi wa umma katika maeneo mbalimbali nchini’amesema Waziri Prof Mbarawa

Mbali na hilo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) sehemu ya kwanza inayoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro (Km 300) Prof. Mbarawa amesema kuwa majaribio ya reli hiyo yanatarajiwa kuanza Mwezi Septemba, mwaka huu.

Hata hivyo wakati Profesa Mbarawa akivitaja vipaumbele vya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23 amesema vipaumbele vingine kuwa ni ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa km 3.2 Jijini Mwanza, kukamilisha Daraja la Wami linalounganisha Mkoa wa Pwani na Tanga, na Ujenzi wa Barabara za kupunguza msongamano na magari yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam na Barabara za mzunguko jijini Dodoma.

By Jamhuri