Dalili za ushindi wa Vladimir Putin wa upande mmoja kama Rais wa Urusi ni dhahiri.

Wasimamizi wa uchaguzi wametangaza kuwa alipata zaidi ya asilimia 87 ya kura katika matokeo yaliyotolewa kufikia sasa.

Putin amekuwa akisema kila mara kuwa ana uhakika wa kuchukua kiti cha urais kwa muhula wa tano.

Kufuatia tangazo la maafisa wa uchaguzi, Putin alitoa maoni kwamba demokrasia ya Urusi iko wazi zaidi kuliko katika nchi nyingi za Magharibi.

Hata hivyo, hakuna kiongozi mwenye nguvu wa upinzani aliyeweza kugombea uchaguzi huo dhidi ya Putin.

Nchi za Magharibi zilishutumu uchaguzi nchini Urusi kwa kutokuwa huru na wa