RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amewatahadharisha wahusika wa shambulizi lililowaua watu zaidi ya 115 eneo la Crocus City Hall nchini humo kuwa atakumbana na adhabu kali.

Akihutubia taifa hilo muda mchache uliopita, Putin amesisitiza kuanzia aliyewatuma hadi waliotekeleza uhalifu huo watashughulikiwa.

Amesema nguvu kubwa inaelekezwa kuwazuia walio nyuma ya shambulizi hilo wasifanye uhalifu mwingine hata hivyo ametoa pole walioguswa na kuumizwa na vifo na majeruhi.

Kikundi cha ISIS kimedai kuhusika na tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo ambapo watu walioficha sura zao waliwashambulia jengo hilo.