Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mtawala wa Mji wa Serikali wa Sejong, Mhe. Kim Hyung- ryeol mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Jeshi wa Seoul, Jamhuri ya Korea kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kikazi tarehe 31 Mei, 2024. Jiji hilo la Sejong ni Makao Makuu Mapya ya Korea Kusini na Jiji hilo lina mahusiano na Jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya Serikali.